naQonda

CBC Grade 8 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 9

c) Maudhui gani yamejitokeza kwenye sehemu hii. Eleza (Alama 3)

From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 1) · 3 marks · Topic: Fasihi, Maudhui

ZOEZI LA 3: NOVELA/RIWAYA (Alama 10)
Soma sehemu ifuatayo kisha ujibu maswali.
Herina aliyasikiliza maneno ya mama yake huku ameinamisha uso wake ulojaa huzuni. Kwa mbali aliona machozi yaliyokuwa yanamlengalenga mamake machoni. Mamake alijaribu kuyaficha machozi hayo lakini yalikataa kufichika. Yalianza kumtiririka njia nnenne huku akiyapangusa kwa leso aliyekuwa amejifunga kiunoni. Herina alitaka kusema jambo ila ulimi wake ulisita. Aliyarudia maneno ya mama yake akilini mwake kana kwamba alitaka kuyaelewa vyema zaidi.

“Mwanangu,” Herina alisikia sauti ya mama yake tena, “Usiyakaidi maneno tuliyoambiwa. Si kwamba hatutaki uendelee na masomo yako lakini uonavyo, hali yetu wazee wako ndiyo hiyo. Tumejikuna tujipatapo hata ukayakamilisha masomo yako ya kiwango hiki. Sitamudu kukukidhia mahitaji ya kujiunga na hiyo shule ya bweni wanayokutaka ujiunge nayo. Linalobaki ni kumshukuru mwenyezi Mungu kwa yote ambayo ametujalia.”

Herina alimkazia mama yake macho yenye haya. Hakujua amwambie nini. Hakujua kilichomfanya mama yake kuamua kuridhi ombi la shangazi yake Dina. Mwenyewe alikuwa amefanya vyema katika tathmini ya kitaifa ya Gredi ya sita. Alikuwa na matumaini ya kijiunga na shule ya upili. Sasa haya yalikuwa yanaelekea kuwa ndoto ambayo isingeweza kutabirika.

“Mama, ninachelea kuwakosea heshima nyingi wazee wangu ila nashangaa vipi shangazi anataka kunitoa huku nyumbani. Kwanini anataka kuniingiza kwenye ajira, mtoto mdogo kama mimi, hata ubwabwa wa shingo haujanitoka? Hata kama ni ajira, kwanini asisubiri mimi mwenyewe nijichagulie baada ya kufika umri wa kufanya kazi za ajira?” Herina alimuuliza mama yake huku machozi yakimlengalenga machoni.

c) Maudhui gani yamejitokeza kwenye sehemu hii. Eleza (Alama 3)

Answer

Umaskini: wazazi hawana uwezo wa kumpeleka Herina shule ya bweni. Ajira ya watoto: shangazi anataka Herina aingie kazini akiwa mdogo. Elimu: Herina anataka kuendelea na masomo.

Taja maudhui na uyaeleze kwa mifano.

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 8 Kiswahili questions from this test