naQonda

CBC Grade 8 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 14

d) Kinyume cha neno 'mnyonge' ni (Alama 1)

From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 1) · 1 mark · Topic: Fasihi, Msamiati

ZOEZI LA 4: TAMTHILIA (Alama 10)
(Siku ya pili. Adhuhuri Mabula na Temba wamekutana mahali pale pale mkahawani. Wote wanakunywa chai kwa vitafunio)
Temba: Wiki imekuwaje?
Mabula: Imenipeleka vizuri.
Temba: (Akipiga funda la chai). Basi nina habari nzuri kwako. Nimesikia kwamba watakurudisha kazini.
Mabula: (Kwa mchangao) Kwa misingi gani?
Temba: Halmashauri kuu imegundua kwamba kosa lilifanyika.
Mabula: Halafu?
Temba: Halafu mameamua urudi kazini.
Mabula: Alaa! Hivyo tu?
Temba: Hivyo tu
Mabula: Hawana hata pole ya kunipaa?
Temba: Labda watafanya japa ninajua hilo ni nadra kutoka kwa mwenye nguvu.
Mabula: Watu hao wote sampuli moja. Baada ya madhila niliyoyapitia hamna hata pole?
Temba: Mabula, pole haiponyi japo ni muhimu. Wewe rejea kama zamani. Una mke na mtoto wanaokutegemea. Hata mwenyewe unahitaji pato walau dogo la kujikimu na familia yako. Kumbuka, mnyonge hana haki.
Mabula: Mnyonge kupata mwenye nguvu kupenda.
Temba: Sawa kabisa.
Mabula: Temba!
Temba: Naam!
Mabula: Hali itakuwa hivi mpaka lini? Lazima awepo mtu wakuwajibika.
Temba: Inafaa hivyo lakini hivi ndivyo ilivyo. Utafanya nini Mabula na una mahitaji.
Mabula: Ina maana tuwe watumwa katika nchi yetu?
Temba: Mabula, sijui kwa nini hautaki kuelewa. Siku zote mhitaji ni mtumwa.
Mabula: (Shingo upande) Haya Tembo.
Temba: (Baada ya kusafisha koo) Mabula ninajua umepitia hali ngumu muda huu ambao umekua huna ajira, lakini hongera kwa kujitahidi.
Mabula: (Anacheka kicheko kirefu kiasi) Huwezi kuelewa.
Temba: Siwezi kuelewa nini?
Mabula: Kuwa hali yangu bado ni ngumu na sijapata habari rasmi.

d) Kinyume cha neno 'mnyonge' ni (Alama 1)

Answer

Mwenye nguvu

Mnyonge ni mtu dhaifu; kinyume ni mwenye nguvu.

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 8 Kiswahili questions from this test