naQonda

CBC Grade 8 Kiswahili Exam Term 3 · Question 1

Chagua jibu sahihi kulingana na aya ya pili.

From Kiswahili Karatasi ya 1 · 1 mark · Topic: Kusoma na Matumizi ya Lugha, Ufahamu na Sarufi

Je, umewahi kuwazia kuhusu usafi wa sehemu za umma? Ama tuseme mazingira yetu kwa jumla? Ama usafi wa kibinafsi? Usafi ni neno ambalo limetawala vinywa vya watu wengi.
Mazingira yanajumuisha makazi yetu, nchi kavu, majini na hata hewani. Manufaa atakayopata mwanadamu kutokana na mazingira yetu yanategemea namna anavyodumisha usafi.
Wazia namna hali ingekuwa bila miti, mito, maziwa, milima, mabonde na hata hewa safi. Yakini hali ingekuwa tata. Kwa mfano, maziwa yakichafuliwa pamoja na mito hali itakuwaje? Mazingira safi yana tija kubwa kwa binadamu. Maji huhitajika viwandani, kunyunyizia mimea, kunywewa na mifugo pamoja na binadamu na vilevile hutumika katika shughuli mbalimbali za nyumbani kama vile za upishi. Maji yasiyokuwa safi huhatarisha maisha.
Mazingira yetu huwa na miti ambayo hurembesha nchi, hutumiwa kwa ujenzi, kutengeneza dawa, huwa makao ya baadhi ya wanyama na vilevile huvuta mvua na kusafisha hewa. Miti huzuia mmomonyoko wa udongo.
Tusitupe taka ovyo wala vitu vinavyoweza kuchafua mazingira. Tukiendelea kufanya hivyo tutakuwa chachandu anayejipalia makaa. Ni muhimu kuthamini usafi wa mazingira.

Chagua jibu sahihi kulingana na aya ya pili.

  1. AWatu wengi hupendezwa na usafi wa mazingira.
  2. BMwanadamu atanufaika na mazingira iwapo atayatunza.
  3. CMakazi yetu na nchi kavu huyatawala mazingira.
  4. DHewa huboresha maisha ya mwanadamu.

Answer

B. Mwanadamu atanufaika na mazingira iwapo atayatunza.

Jibu sahihi ni: Mwanadamu atanufaika na mazingira iwapo atayatunza.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 8 Kiswahili questions from this test