CBC Grade 7 Kiswahili Opener Exam Term 3 · Question 23
Vipengele vifuatavyo vya Kusikiliza na Kuzungumza vimebainika katika mazungumzo haya isipokuwa:
From Test 1 — Opener Exam Term 3 (702/1: Kiswahili Lugha) · 1 mark · Topic: Kusikiliza na Kuzungumza, Stadi za Kusikiliza na Kuzungumza
Kifungu cha Tano: Mazungumzo kati ya Bi. Amina na Bi. Nuru
(Ni alasiri. Jua linakaribia kuzama. Bi. Amina ameketi kwenye kiti nje ya nyumba yake, akifua nguo. Jirani yake, Bi. Nuru, anapita akielekea shambani kwake. Anamwona Bi. Amina.)
Bi. Nuru: Jirani, habari za alasiri? Nakuona bado unaendelea na shughuli zako.
Bi. Amina: (Akiinua kichwa na kutabasamu) 21______________ jirani. Kazi haziishi. Leo nimeamua kufua nguo zote kabla ya mvua kunyesha.
Bi. Nuru: Ndio maana nimekuona hapa kwa muda. (Kwa huruma) Ni kweli, hali ya hewa inabadilika. Mvua ikinyesha ghafla, itakuharibia kazi.
Bi. Amina: Kweli kabisa. Ninahitaji kumaliza haraka.
Bi. Nuru: Juzi nimekuona ukiuguza mtoto. Amepona?
Bi. Amina: Ah, mtoto amepona sasa. Ni homa tu ilikuwa ikimsumbua. Nashukuru Mungu.
Bi. Nuru: Nashukuru kusikia hivyo. Afya njema ni muhimu.
Bi. Amina: Kweli kabisa. Sasa wewe unaelekea wapi, jirani?
Bi. Nuru: Ninaelekea shambani kwangu. Ninahitaji kukagua mazao yangu. Hali ya hewa imekuwa ikitishia, hivyo nina wasiwasi na mimea yangu.
Bi. Amina: Nakuelewa. Mungu akubariki katika kazi zako.
Bi. Nuru: Asante, jirani. Nakutakia jioni njema. (Anamwaga) 25____________________.
(Bi. Nuru anaendelea na safari yake huku Bi. Amina akiendelea kufua nguo.)

- AKutumia lugha ya adabu.
- BKujibu maswali kwa ukamilifu.
- CKukatiza mzungumzaji mwingine.
- DKubadilishana zamu za kuzungumza.
Answer
C. Kukatiza mzungumzaji mwingine.
Jibu sahihi: Kukatiza mzungumzaji mwingine.
More Grade 7 Kiswahili questions from this test
- Bi. Amina alimsimulia Bi. Nuru kuhusu homa ya mtoto wake. Unadhani Bi. Nuru angetumia neno gani kuonyesha hisia zake…Question 24
- Chagua nahau inayofaa kujaza nafasi ya 25 katika kifungu.Question 25
- Chagua jibu lifaalo zaidi kujaza nafasi ya 26 katika kifungu.Question 26
- Chagua jibu lifaalo zaidi kujaza nafasi ya 27 katika kifungu.Question 27
- Chagua jibu lifaalo zaidi kujaza nafasi ya 28 katika kifungu.Question 28
- Chagua jibu lifaalo zaidi kujaza nafasi ya 29 katika kifungu.Question 29