CBC Grade 7 Kiswahili Exam Term 1 2025 · Question 1
Je, ni kweli kusema binadamu wote wanakubaliana kwa kauli moja kuwa wimbo Fulani ndio bora? (Ndio au La) (al 1)
From Kiswahili — Extra-Activity Assessment 2025 (Set 8) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
A. UFAHAMU
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 1 hadi la 5.
Umuhimu wa muziki hasa ni nini? Watunzi wa nyimbo mbalimbali huwa wana msukumo upi? Lengo lao huwa lipi? Ni mambo yapi hutazamwa kabla ya wimbo Fulani kupigwa debe kuwa ni mzuri?
Najua vyema kuwa ni muhali binadamu wote katika mazingira yoyote yale kuungana kwa asilimia mia kuwa wimbo fulani ndio bora. Ndimi za wanadamu huona utamu mbalimbali katika chakula kimoja. Vivyo hivyo masikio na akili.
Hata hivyo wimbo mzuri lazima uwe na lengo Fulani la kutimizwa linalokubaliwa katika jamii. Kinachoshangaza siku hizi ni nyimbo za kisiasa. Nyingi hazina hata chembe ya maadili. Lugha si lugha. Baadhi ya video bila kupiga vijembe nina uhakika zilitolewa katika ghala la shetani. Hazitamaniki kamwe. Mtunzi wa nyimbo kama hizi bila shaka nia yake ni kuleta fujo na kuhatarisha amani.
Ni vyema kutunga nyimbo zinazozingatia maadili ya jamii. Hivyo basi serikali na wazalendo wote wapige marufuku nyimbo ambazo hazizingatii maadili na kuleta faida kwa jamii.
1. Je, ni kweli kusema binadamu wote wanakubaliana kwa kauli moja kuwa wimbo Fulani ndio bora? (Ndio au La) (al 1)
Answer
La.
Mwandishi anasema ni muhali binadamu wote kuungana kwa asilimia mia.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 7 Kiswahili questions from this test
- Mwandishi ameuliza maswali mangapi yanayohusiana na muziki katika aya ya kwanza? (al 1)Question 2
- Unafikiria ni kwa nini mwandishi amesema video nyingine zilitolewa katika ghala la shetani? (al 1)Question 3
- Mwisho mwandishi anapendekeza nini kuhusu utunzi wa nyimbo? (al 1)Question 4
- Mwisho mwandishi anapendekeza serikali na wazalendo wote wafanye nini? (al 1)Question 5
- Taja faida mbili za vile tarakilishi imechangia katika ukuaji wa Uchumi. (al 2)Question 6
- Taja njia mbili za vile tarakilishi imeundwa kuiga Mungu. (al.2)Question 7