naQonda

CBC Grade 7 Kiswahili Opener Exam Term 2 2026 · Question 21

Chagua jibu sahihi kujaza pengo la 21.

From Kiswahili — Term 2 Opener Assessment 2026 (Set 12) · 1 mark · Topic: Kusikiliza na Kuzungumza, Ufahamu wa Mazungumzo

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu swali la 18 mpaka la 25
(Ni wakati wa jioni. Baraki amemtembelea Jimi kwao nyumbani)
Baraki: (Akibisha) Hodi!
Jimi: Karibu.
Baraki: (Baada ya kuingia) ___(18)___ rafiki yangu.
Jimi: Akheri. Natumai umeshinda vyema.
Baraki: Naam. Leo hali ilikuwa shwari shuleni. Hata hivyo, wewe hukuweza kufika. Ndiposa nimeamua kuja kukujulia hali.
Jimi: Asante ndugu yangu. Leo mnuna wangu alikuwa akiugua. Ilinibidi nimsaidie mama kumpeleka hospitali kwa baiskeli.
Baraki: Ooh! Pole sana. Je, hali yake iko vipi sasa hivi?
Jimi: (Anatulia kidogo) Asubuhi alikuwa na joto jingi. Aidha alikuwa akiendesha na kutapika. Tulihofu kuwa ni ugonjwa wa ___(21)___ ambao huwa na dalili hizo. Hata hivyo, daktari alimpomchunguza aligundua kuwa anaugua malaria.
Baraki: Heri nusu ya shari kuliko shari kamili. Ugonjwa wa kipindupindu ni hatari sana. Lau ungekuwa huo hali ingekuwa mbaya zaidi.
Jimi: Visa vya maambukizi ya malaria huongezeka katika msimu wa masika. Hii ni kwa sababu mbu huzaana kwa wingi.
Baraki: Mlipata huduma mlizohitaji hospitalini?
Jimi: Naam, mdogo wangu alipewa dawa za kumeza. Mama alipewa chandarua kilichotibiwa ili awe akimlaza hapo. Kwa bahati nzuri, familia yangu imejisajili katika bima ya afya. Hatukulipia chochote kwa huduma hiyo.
Baraki: Asante ndugu yangu. Kwa kuwa kesho ni siku ya Jumamosi, nitakusaidia kufyeka vichaka hivi na kuondoa mikebe iliyo karibu. Au waonaje?
Jimi: Hapo ni sawa. Karibu sana.
Baraki: ___(25)___ rafiki yangu. Hebu niende nimsaidie mama kuandaa chajio.
Jimi: Binuru. Tutaonana kesho Mungu akipenda.

21. Chagua jibu sahihi kujaza pengo la 21.

  1. Autapiamlo
  2. Bkichocho
  3. Cwaba
  4. Dmalale

Answer

C. waba

Kuendesha na kutapika ni dalili za kipindupindu, ambacho pia huitwa waba — Baraki anasema "Ugonjwa wa kipindupindu ni hatari sana." Malale ni ugonjwa wa usingizi unaoenezwa na mbung'o.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 7 Kiswahili questions from this test