CBC Grade 7 Kiswahili Opener Exam Term 2 2026 · Question 25
Jaza nafasi ya 25 kwa usahihi.
From Kiswahili — Term 2 Opener Assessment 2026 (Set 12) · 1 mark · Topic: Kusikiliza na Kuzungumza, Ufahamu wa Mazungumzo
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu swali la 18 mpaka la 25
(Ni wakati wa jioni. Baraki amemtembelea Jimi kwao nyumbani)
Baraki: (Akibisha) Hodi!
Jimi: Karibu.
Baraki: (Baada ya kuingia) ___(18)___ rafiki yangu.
Jimi: Akheri. Natumai umeshinda vyema.
Baraki: Naam. Leo hali ilikuwa shwari shuleni. Hata hivyo, wewe hukuweza kufika. Ndiposa nimeamua kuja kukujulia hali.
Jimi: Asante ndugu yangu. Leo mnuna wangu alikuwa akiugua. Ilinibidi nimsaidie mama kumpeleka hospitali kwa baiskeli.
Baraki: Ooh! Pole sana. Je, hali yake iko vipi sasa hivi?
Jimi: (Anatulia kidogo) Asubuhi alikuwa na joto jingi. Aidha alikuwa akiendesha na kutapika. Tulihofu kuwa ni ugonjwa wa ___(21)___ ambao huwa na dalili hizo. Hata hivyo, daktari alimpomchunguza aligundua kuwa anaugua malaria.
Baraki: Heri nusu ya shari kuliko shari kamili. Ugonjwa wa kipindupindu ni hatari sana. Lau ungekuwa huo hali ingekuwa mbaya zaidi.
Jimi: Visa vya maambukizi ya malaria huongezeka katika msimu wa masika. Hii ni kwa sababu mbu huzaana kwa wingi.
Baraki: Mlipata huduma mlizohitaji hospitalini?
Jimi: Naam, mdogo wangu alipewa dawa za kumeza. Mama alipewa chandarua kilichotibiwa ili awe akimlaza hapo. Kwa bahati nzuri, familia yangu imejisajili katika bima ya afya. Hatukulipia chochote kwa huduma hiyo.
Baraki: Asante ndugu yangu. Kwa kuwa kesho ni siku ya Jumamosi, nitakusaidia kufyeka vichaka hivi na kuondoa mikebe iliyo karibu. Au waonaje?
Jimi: Hapo ni sawa. Karibu sana.
Baraki: ___(25)___ rafiki yangu. Hebu niende nimsaidie mama kuandaa chajio.
Jimi: Binuru. Tutaonana kesho Mungu akipenda.
25. Jaza nafasi ya 25 kwa usahihi.
- AKwaheri
- BTuonane kesho
- CAlamsiki
- DBuriani
Answer
C. Alamsiki
Jimi anajibu "Binuru", ambalo ni jibu la "Alamsiki" — maagano ya jioni au usiku. "Kwaheri" hujibiwa "Kwaheri ya kuonana".
More Grade 7 Kiswahili questions from this test
- Chagua jibu linalofaa kujaza nafasi ya 26.Question 26
- Chagua jibu linalofaa kujaza nafasi ya 27.Question 27
- Chagua jibu linalofaa kujaza nafasi ya 28.Question 28
- Chagua jibu linalofaa kujaza nafasi ya 29.Question 29
- Chagua jibu linalofaa kujaza nafasi ya 30.Question 30
- Chagua jibu linalofaa kujaza nafasi ya 31.Question 31