naQonda

CBC Grade 7 Kiswahili Opener Exam Term 2 2026 · Question 15

Aya ya tatu inaonyesha

From Kiswahili — Term 2 Opener Assessment 2026 (Set 12) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Makala

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 10 mpaka la 17.
Wanajamii wote wanafaa kuzingatia maadili bila kujali umri, jinsia, dini wala tabaka. Sharti ieleweke kwamba katika jamii inayopuuza maadili, maovu ainati hushamiri. Ustawi wa jamii yoyote ile hutegemea jinsi shughuli katika jamii hiyo zinavyoendeshwa kwa uadilifu.
Watoto hujifunza mengi kutoka kwa wavyele wao na jamaa wengine wa umri mbalimbali wanaotangamana nao kila siku. Ikiwa, kwa mfano, mzazi ni mlevi, mwizi au anatumia lugha ya ufidhuli, haitashangaza mtoto wake akiwa na mienendo iyo hiyo. Chambilecho wahenga mwana wa ndovu hawi mkovu. Kwa upande mwingine, mzazi au mlezi akionyesha unyenyekevu, uaminifu na upendo kwa wanajamii wenzake, mustakabali wa mwanawe utakuwa mzuri kwani ataiga mienendo iyo hiyo.
Mazingira ya mtoto nayo huwa na mchango usioweza kupuuzwa katika maisha yake. Vipindi vya runinga, matukio ya shuleni, kijijini au mjini anakolelewa mtoto humwathiri kwa namna mbalimbali maishani. Ikiwa mtoto ataonyeshwa kuwa njia ya pekee ya kutatua migogoro ni kwa mtutu wa bunduki, au magumi na mateke, tusimtarajie atumie njia za utulivu katika kufikia haki zake. Siku zote atakuwa akijua kwamba dawa ya moto ni moto. Atadai haki zake kwa njia za kimabavu.
Ni vyema tuzingatie maadili ya kibinafsi na kijamii popote pale tulipo. Kazi ya mambo tunayotarajiwa kufanya ni kuheshimu mali ya wengine, kuzingatia bidii, kuonyesha upendo kwa wengine, kujaliana maslahi na kuheshimiana. Uwajibikaji wetu hao uwe dhahiri popote tulipo; yaani shuleni, kazini, shambani na hata njiani tunapotembea.

15. Aya ya tatu inaonyesha

  1. Aathari ya mazingira katika malezi ya mtoto
  2. Bmchango wa shule katika maisha ya mtoto
  3. Cnjia mbalimbali za kutatua mizozo
  4. Dmtoto afunzwe kutafuta haki kwa nguvu.

Answer

A. athari ya mazingira katika malezi ya mtoto

Aya ya tatu inaanza: "Mazingira ya mtoto nayo huwa na mchango usioweza kupuuzwa katika maisha yake."

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 7 Kiswahili questions from this test