CBC Grade 7 Kiswahili School Based Assessment 2025 · Question 15
(c) Eleza umuhimu wa maelezo yaliyoandikwa kwa herufi za mlazo katika sehemu hii ya tamthilia. (alama 2)
From Kiswahili — KJSEA Series July–August 2025 (Set 12) · 2 marks · Topic: Kusoma, Tamthilia
4. Soma sehemu ifuatayo ya tamthilia kisha ujibu maswali.
SEHEMU 1
Onyesho 1
(Ni katika uwanja wa shule ya Msingi Majengo. Wanafunzi wamekusanyika wakiwa na vitabu na madaftari. Baadhi wamekaa kwenye madawati ya nje, wengine chini ya mti mkubwa. Mwalimu Pendo, mwalimu wa Kiswahili, anaingia akiwa amebeba rundo la vitabu.)
Mwalimu Pendo: (Kwa sauti ya upole) Habari zenu wanafunzi wangu?
Wanafunzi: (Kwa sauti moja) Nzuri sana Mwalimu!
Mwalimu Pendo: Hongereni kwa bidii yenu. Leo tuna somo muhimu sana. Nataka tuzungumzie umuhimu wa usafi wa mazingira.
Mwenda: (Akinyosha mkono) Mwalimu, nina swali.
Mwalimu Pendo: Uliza Mwenda.
Mwenda: Kwa nini usafi ni muhimu sana, hasa hapa shuleni?
Mwalimu Pendo: (Akitabasamu) Swali zuri sana Mwenda. Usafi ni nguzo muhimu ya afya yetu na ya jamii. Hebu fikiria shule chafu. Mtaweza kusoma vizuri?
Kituo: La hasha Mwalimu. Wadudu na maradhi yataenea.
Mwalimu Pendo: Sahihi kabisa Kituo. Na si shuleni pekee. Hata nyumbani na katika jamii zetu. Kuna methali isemayo, Usafi ni nusu ya imani. Ni muhimu kuishi katika mazingira safi. Tunaweza kufanya nini ili kudumisha usafi?
Jua: Tunaweza kufagia madarasa yetu kila siku.
Mwalimu Pendo: Vizuri Jua. Nani mwingine?
Raha: Kutupa taka kwenye mapipa ya taka.
Mwalimu Pendo: (Akipiga makofi) Hongera Raha! Mna mawazo mazuri sana. Kila mmoja wetu ana jukumu la kuhakikisha mazingira yetu ni safi. Hata michezo yetu lazima idumishwe usafi. Tusisahau kuwa sisi ndio walinzi wa dunia yetu.
(Ghafla, kengele ya mapumziko inalia. Wanafunzi wanainuka na kuanza kujipanga.)
(c) Eleza umuhimu wa maelezo yaliyoandikwa kwa herufi za mlazo katika sehemu hii ya tamthilia. (alama 2)
Answer
Yanamwelekeza mwigizaji jinsi ya kutenda au kuzungumza, kwa mfano (Kwa sauti ya upole), na yanaeleza mandhari na matukio, kama (Ghafla, kengele ya mapumziko inalia).
Maelekezo ya jukwaa yanaonyesha jinsi ya kutenda na kuzungumza, hisia za wahusika, mandhari na mabadiliko ya matukio.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 7 Kiswahili questions from this test
- (d) Neno ‘nguzo’ ni mfano wa mbinu ya nahau. Eleza mbinu nyingine mbili za lugha zilizotumiwa katika sehemu hii ya…Question 16
- ZOEZI V: USHAIRI (Alama 5) (a) Eleza ujumbe wa shairi hili. (Alama 1)Question 17
- (b) Shairi hili lina beti ngapi? (Alama 1)Question 18
- (c) Taja aina moja ya teknolojia iliyotajwa kwenye shairi. (Alama 1)Question 19
- (d) Malenga kwenye shairi hili ni nani? (alama 1)Question 20
- (e) Andika mshororo wa mwisho katika beti ya tano. (alama 1)Question 21