CBC Grade 7 Kiswahili School Based Assessment 2025 · Question 21
(e) Andika mshororo wa mwisho katika beti ya tano. (alama 1)
From Kiswahili — KJSEA Series July–August 2025 (Set 12) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ushairi
5. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali
SHAIRI: ELIMU NI NURU
1. Elimu ni nuru, twaifuate sote,
Maishani mwetu, itatuongoza kweli,
Tujitahidi sana, tusicheze na kutega,
Maarifa ni hazina, yenye thamani tele.
2. Shuleni twaenda, kupata maarifa,
Walimu hufundisha, kwa bidii na juhudi,
Tusikose kuandika, na kuzingatia daima,
Kila somo ni muhimu, litatujenga akili.
3. Hisabati ngumu, haitupi shida sisi,
Sayansi ya maumbile, yatufungua macho,
Kiswahili chetu, lugha yetu tamu sana,
Kufahamu mengi, ni jambo la busara.
4. Teknolojia mpya, twaifahamu vema,
Kompyuta na intaneti, zimetuletea mbali,
Dunia imebadilika, tunahitaji kujua,
Kujitegemea maishani, ndio lengo kuu.
5. Tujifunze na kucheza, tusisahau michezo,
Afya njema ni muhimu, kwa mwili na akili,
Kudumisha nidhamu, ni msingi wa mafanikio,
Heshima kwa wote, sifa njema tutapata.
6. Tujiandae kwa kesho, tufungue milango,
Kazi nyingi zadai, elimu ya hali ya juu,
Madaktari na marubani, walimu na wahandisi,
Yote haya yahitaji, maarifa siyo ya kujuakujuwa.
7. Hivyo basi wanafunzi, tujitoe kwa moyo,
Elimu ni ufunguo, wa kufungua ulimwengu,
Tufanye bidii zetu, tusipoteze muda,
Mafanikio ni yetu, tukichapa kazi kweli.
(K. David)
(e) Andika mshororo wa mwisho katika beti ya tano. (alama 1)
Answer
Heshima kwa wote, sifa njema tutapata.
Ubeti wa tano unaanza "Tujifunze na kucheza" na mshororo wake wa mwisho ni "Heshima kwa wote, sifa njema tutapata."
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 7 Kiswahili questions from this test
- SEHEMU A (Alama 15) ZOEZI I: INSHA Maagizo i. Inapendekezwa uchukue muda wa dakika 40 katika zoezi hili. ii. Andika…Question 1
- SEHEMU B (Alama 35) ZOEZI II: FASIHI SIMULIZI (Alama 10) (a) Kipera cha hadithi hii ni nini? Toa sababu moja…Question 2
- (b) Eleza sifa mbili za Mzee Kobe kama zinavyojitokeza katika hadithi hii. (alama 2)Question 3
- (c) Ni ujumbe gani mkuu unapatikana katika hadithi ya Mzee Kobe? (alama 1)Question 4
- (d) Taja mbinu mbili za uwasilishaji ambazo Mzee Kobe alizitumia ili kuwafunza wanakijiji. (alama 2)Question 5
- (e) Kauli, ‘Mwalimu wa Maisha’ imetumiwa katika hadithi hii. Eleza maana yake kulingana na muktadha wa hadithi. (alama…Question 6