CBC Grade 7 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 24
Chagua neno ambalo Tunda angetumia katika nafasi ya 24 kwenye mazungumzo.
From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 5) · 1 mark · Topic: Kusikiliza na Kuzungumza, Mazungumzo
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 21 hadi la 25.
(Ni katika uwanja wa shule. Wanafunzi wanafanya mazoezi ya michezo. Tunda na bwana mdogo Zawadi wanapiga mpira huku wakizungumza.)
Tunda: (Akimsogelea.) Hali gani Zawadi?
Zawadi: Salama kabisa ndugu yangu. Nawe unaendeleaje na mazoezi yako?
Tunda: (Akicheka.) ___21___ Najitayarisha kwa mashindano ya wilaya. Timu yetu inajikaza sana. Unajua, jitihada haiondoi...
Zawadi: (Akimalizia.) Kudura, ni kweli. Sisi pia tunafanya kazi kwa bidii. Mwaka jana tulishindwa, lakini safari hii tumeamua liwe liwalo, ushindi ni wetu.
Tunda: (Akitupa mpira.) Safi! Hata upande wa wasichana, wameamua kuwa mwaka huu lazima wanyakue kombe.
Zawadi: (Akisimama.) Ngoja nipumzike. Nimechoka sana na miguu inaniuma. Nikiendelea hivi nitaumia.
Tunda: (Akijinyoosha.) ___24___ Kweli kabisa, mwili unahitaji utulivu. Kwaheri. Tutaonana darasani punde.
Zawadi: (Akimpungia mkono.) Nami nitakuja huko sasa hivi. (Wanaagana.)
24. Chagua neno ambalo Tunda angetumia katika nafasi ya 24 kwenye mazungumzo.
- ABasi
- BPole
- CKunradhi
- DHongera
Answer
A. Basi
"Basi" hukubali na kufunga mazungumzo.
More Grade 7 Kiswahili questions from this test
- Ni ishara gani ambayo Zawadi alistahili kutumia alipomuaga Tunda?Question 25
- Chagua jibu lifaalo zaidi kujaza nafasi 26.Question 26
- Chagua jibu lifaalo zaidi kujaza nafasi 27.Question 27
- Chagua jibu lifaalo zaidi kujaza nafasi 28.Question 28
- Chagua jibu lifaalo zaidi kujaza nafasi 29.Question 29
- Chagua jibu lifaalo zaidi kujaza nafasi 30.Question 30