CBC Grade 7 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 12
Chagua jibu ambalo si kichwa mwafaka kwa kifungu hiki.
From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 5) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali ya 7 hadi 12.
Kijana mmoja aliitwa Juma alikuwa akielekea mjini. Njiani, alikutana na mtu mzima aliyeitwa Bwana Janja. "Hujambo mjukuu? Nina shida kubwa," Bwana Janja alisema kwa haraka. "Nataka kulipa nauli ya basi lakini nina noti ya elfu moja pekee. Naomba unibadilishie nipate pesa ndogondogo".
Juma alikuwa amesikia kuwa Bwana Janja ni mtu mlaghai anayependa kudanganya watoto. Hata hivyo, aliamua kumsaidia na kumpa noti mbili za mia tano. Bwana Janja alizichukua pesa zile na kutokomea upesi. Baadaye, Juma aliende dukani kununua kalamu. Muuzaji alimwambia, "Pesa hii ni bandia! Ni karatasi tu". Juma alishangaa lakini hakulia. Alielekea kule Bwana Janja alipokuwa akiwaibia watu kwa michezo ya kamari.
Juma alichukua simu yake na kuwapigia maafisa wa usalama. Alijifanya anataka kucheza mchezo huo kwa kutumia ile pesa bandia. Bwana Janja alicheka akifikiri amempata mjinga mwingine. Ghafla, maafisa walifika na kumkamata. Juma alitabasamu kuona kuwa ujanja wa Bwana Janja umefika kikomo.
12. Chagua jibu ambalo si kichwa mwafaka kwa kifungu hiki.
- AUjanja wa Bwana Janja.
- BUmhimu wa kutoa ripoti polisi.
- CManufaa ya kucheza kamari barabarani.
- DMadhara ya udanganyifu katika jamii.
Answer
C. Manufaa ya kucheza kamari barabarani.
Kifungu hakisifu kamari.
More Grade 7 Kiswahili questions from this test
- Kulingana na kifungu hiki, ___Question 13
- Kuwafundisha watoto kutunza usafi ni njia moja ya kukuza___Question 14
- Chagua jibu ambalo ni sahihi kwa mujibu wa kifungu.Question 15
- Ukiukaji wa sheria za mazingira husababishaQuestion 16
- Kulingana na kifungu, maana ya neno 'maisha ya baadaye' (mustakabali) niQuestion 17
- Chagua jibu linaloonyesha klabu ambazo wanafunzi hukutana mara mbili pekee kwa juma.Question 18