naQonda

CBC Grade 7 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 11

Chagua methali inayoweza kutumiwa kumshauri Bwana Janja.

From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 5) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali ya 7 hadi 12.
Kijana mmoja aliitwa Juma alikuwa akielekea mjini. Njiani, alikutana na mtu mzima aliyeitwa Bwana Janja. "Hujambo mjukuu? Nina shida kubwa," Bwana Janja alisema kwa haraka. "Nataka kulipa nauli ya basi lakini nina noti ya elfu moja pekee. Naomba unibadilishie nipate pesa ndogondogo".
Juma alikuwa amesikia kuwa Bwana Janja ni mtu mlaghai anayependa kudanganya watoto. Hata hivyo, aliamua kumsaidia na kumpa noti mbili za mia tano. Bwana Janja alizichukua pesa zile na kutokomea upesi. Baadaye, Juma aliende dukani kununua kalamu. Muuzaji alimwambia, "Pesa hii ni bandia! Ni karatasi tu". Juma alishangaa lakini hakulia. Alielekea kule Bwana Janja alipokuwa akiwaibia watu kwa michezo ya kamari.
Juma alichukua simu yake na kuwapigia maafisa wa usalama. Alijifanya anataka kucheza mchezo huo kwa kutumia ile pesa bandia. Bwana Janja alicheka akifikiri amempata mjinga mwingine. Ghafla, maafisa walifika na kumkamata. Juma alitabasamu kuona kuwa ujanja wa Bwana Janja umefika kikomo.

11. Chagua methali inayoweza kutumiwa kumshauri Bwana Janja.

  1. AMtoto wa nyoka ni nyoka.
  2. BAsiyesikia la mkuu huvunjika guu.
  3. CMvumilivu hula mbivu.
  4. DSiku za mwizi ni arobaini.

Answer

D. Siku za mwizi ni arobaini.

Mdanganyifu hukamatwa siku moja.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 7 Kiswahili questions from this test