CBC Grade 7 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 8
Ni jibu lipi linaloonyesha uhusiano uliopo kati ya Juma na Bwana Janja?
From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 5) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali ya 7 hadi 12.
Kijana mmoja aliitwa Juma alikuwa akielekea mjini. Njiani, alikutana na mtu mzima aliyeitwa Bwana Janja. "Hujambo mjukuu? Nina shida kubwa," Bwana Janja alisema kwa haraka. "Nataka kulipa nauli ya basi lakini nina noti ya elfu moja pekee. Naomba unibadilishie nipate pesa ndogondogo".
Juma alikuwa amesikia kuwa Bwana Janja ni mtu mlaghai anayependa kudanganya watoto. Hata hivyo, aliamua kumsaidia na kumpa noti mbili za mia tano. Bwana Janja alizichukua pesa zile na kutokomea upesi. Baadaye, Juma aliende dukani kununua kalamu. Muuzaji alimwambia, "Pesa hii ni bandia! Ni karatasi tu". Juma alishangaa lakini hakulia. Alielekea kule Bwana Janja alipokuwa akiwaibia watu kwa michezo ya kamari.
Juma alichukua simu yake na kuwapigia maafisa wa usalama. Alijifanya anataka kucheza mchezo huo kwa kutumia ile pesa bandia. Bwana Janja alicheka akifikiri amempata mjinga mwingine. Ghafla, maafisa walifika na kumkamata. Juma alitabasamu kuona kuwa ujanja wa Bwana Janja umefika kikomo.
8. Ni jibu lipi linaloonyesha uhusiano uliopo kati ya Juma na Bwana Janja?
- AWalikuwa marafiki wanaopendana sana.
- BBwana Janja alikuwa mwalimu wa Juma.
- CJuma alikuwa amesikia sifa mbaya za Bwana Janja.
- DWalikuwa wakishirikiana katika michezo ya kamari.
Answer
C. Juma alikuwa amesikia sifa mbaya za Bwana Janja.
Juma alikuwa amesikia kuwa ni mlaghai.
More Grade 7 Kiswahili questions from this test
- Neno 'ulaghai' limetumiwa katika kifungu. Chagua kisawe cha neno hilo.Question 9
- Je, unafikiri Bwana Janja alifanya nini baada ya kukamatwa na maafisa?Question 10
- Chagua methali inayoweza kutumiwa kumshauri Bwana Janja.Question 11
- Chagua jibu ambalo si kichwa mwafaka kwa kifungu hiki.Question 12
- Kulingana na kifungu hiki, ___Question 13
- Kuwafundisha watoto kutunza usafi ni njia moja ya kukuza___Question 14