naQonda

CBC Grade 7 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 23

Ni kipi hasa kilimfanya mzee kobe kuchukua umbo la kikobe?

From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 3) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu

Soma habari ifuatayo kisha uyajibu maswali nambari ya 20 hadi 25.
Siku moja Emili alipokuwa akielekea mtoni kuchota maji, alikutana na maajabu makubwa. Njiani alikutana na mzee kobe ambaye alikuwa akisoma. Mzee kobe alipomuona Emili akipita akamuamkua.
Kwanza Emili aliposikia sauti, hakuweza kuamini kuwa alikuwa ni mzee kobe. Akageuka na kutafutatafuta kule sauti hiyo ilikotokea. Mzee kobe alimgeukia na kuanza kuzungumza na Emili katika mshtuko wake. Mzee kobe: Mbona hutaki kuamini kuwa mimi ndimi ninakuamkua? Au unafikiri mimi sina ulimi wa kuzungumza kama wewe?
Emili: (Huku macho yamemtoka kwa mshangao). Hakika siamini kuwa kobe anaweza kuwa na uwezo wa kusoma kama binadamu na ndio maana hata sasa sijaamini masikio yangu kuwa ni wewe mwenye kusema nami.
Mzee Kobe: Ukweli ni kwamba mimi si kobe! Mimi ni binadamu. Lakini kwa sababu ya tamaa yangu kubwa, ndipo nimejikuta katika umbo la kikobe.
Emili: Unaweza kunifichulia siri yako?
Mzee Kobe: Siwezi kwani nliambiwa kuwa ukiwa nitaifichua siri yangu, basi huenda nikageuka mnyama mbaya zaidi ya kobe na hilo si lengo langu.
Emili: Ninakuomba uniambie ili nipate kuwaambia walimwenu kuwa hii leo nimekutana na kobe mwenye kusema kama binadamu.
Mzee Kobe: La! siwezi, kamwe kukuambia kwani nikifanya hivyo nitaota manyoya na kugeuka kiumbe kibaya zaidi.

23. Ni kipi hasa kilimfanya mzee kobe kuchukua umbo la kikobe?

  1. AMadaha
  2. BBidii
  3. CTamaa
  4. DKurogwa

Answer

C. Tamaa

"Kwa sababu ya tamaa yangu kubwa."

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 7 Kiswahili questions from this test