CBC Grade 7 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 21
Kwa nini kobe alimzungumzia Emili katika mshtuko wake?
From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 3) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma habari ifuatayo kisha uyajibu maswali nambari ya 20 hadi 25.
Siku moja Emili alipokuwa akielekea mtoni kuchota maji, alikutana na maajabu makubwa. Njiani alikutana na mzee kobe ambaye alikuwa akisoma. Mzee kobe alipomuona Emili akipita akamuamkua.
Kwanza Emili aliposikia sauti, hakuweza kuamini kuwa alikuwa ni mzee kobe. Akageuka na kutafutatafuta kule sauti hiyo ilikotokea. Mzee kobe alimgeukia na kuanza kuzungumza na Emili katika mshtuko wake. Mzee kobe: Mbona hutaki kuamini kuwa mimi ndimi ninakuamkua? Au unafikiri mimi sina ulimi wa kuzungumza kama wewe?
Emili: (Huku macho yamemtoka kwa mshangao). Hakika siamini kuwa kobe anaweza kuwa na uwezo wa kusoma kama binadamu na ndio maana hata sasa sijaamini masikio yangu kuwa ni wewe mwenye kusema nami.
Mzee Kobe: Ukweli ni kwamba mimi si kobe! Mimi ni binadamu. Lakini kwa sababu ya tamaa yangu kubwa, ndipo nimejikuta katika umbo la kikobe.
Emili: Unaweza kunifichulia siri yako?
Mzee Kobe: Siwezi kwani nliambiwa kuwa ukiwa nitaifichua siri yangu, basi huenda nikageuka mnyama mbaya zaidi ya kobe na hilo si lengo langu.
Emili: Ninakuomba uniambie ili nipate kuwaambia walimwenu kuwa hii leo nimekutana na kobe mwenye kusema kama binadamu.
Mzee Kobe: La! siwezi, kamwe kukuambia kwani nikifanya hivyo nitaota manyoya na kugeuka kiumbe kibaya zaidi.
21. Kwa nini kobe alimzungumzia Emili katika mshtuko wake?
- AKwa sababu Emili hakuamini kwamba anaweza kukutana na kobe.
- BKwa sababu Emili alishtukiwa kuona kuwa hata kobe anazungumza.
- CKwa sababu mzee kobe alimshtua sana Emili.
- DKwa sababu si rahisi kukutana na kobe.
Answer
B. Kwa sababu Emili alishtukiwa kuona kuwa hata kobe anazungumza.
Emili hakuamini kuwa kobe anaweza kuzungumza.
More Grade 7 Kiswahili questions from this test
- “Huku macho yamemtoka” maana yake niQuestion 22
- Ni kipi hasa kilimfanya mzee kobe kuchukua umbo la kikobe?Question 23
- Mzee kobe aliogopa kufichua siri ya kwa sababuQuestion 24
- Angeifichua siri hii angeotaQuestion 25
- Chagua jibu mwafaka kujaza nafasi 26.Question 26
- Chagua jibu mwafaka kujaza nafasi 27.Question 27