naQonda

CBC Grade 7 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 3

b) Taja mandhari mbili ambayo imejitokeza katika kisa hiki? (Alama 2)

From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 4) · 2 marks · Topic: Kusoma, Fasihi Simulizi

SEHEMU YA B: FASIHI SIMULIZI (ALAMA 10)
Soma kisa kifuatacho kisha ujibu maswali.
Hapo zamani za kale, kuku na mwewe walikuwa marafiki wakubwa. Walipendana kama suruari na tako. Waliishi pamoja porini kwa amani na kusaidiana kutafuta chakula. Mwewe alikuwa karimu sana na kuku alimwamini kwa kila jambo.
Siku moja, kuku alimwomba mwewe amkopeshe nafaka ili awalishe watoto wake. Mwewe alimpa nafaka akamwambia amrejeshee itakayobaki. Kuku alikubali na kuondoka na nafaka.
Hata hivyo, kuku alitumia nafaka yote na kukosa kurudisha. Kila alipoulizwa, alitoa visingizio na kumhepa mwewe. Mwewe alikasirika kwa sababu kuku hakutimiza ahadi yake.
Siku moja, mwewe alimkuta kuku akiwa na vifaranga wake na akasema kuwa atakuwa akichukua vifaranga kama fidia ya nafaka yake. Tangu siku hiyo, mwewe alianza kuwinda vifaranga wa kuku naye kuku akaanza kuwaficha watoto wake kila mara alipomwona mwewe angani.

b) Taja mandhari mbili ambayo imejitokeza katika kisa hiki? (Alama 2)

Answer

Porini na kijijini.

Waliishi wapi?

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 7 Kiswahili questions from this test