CBC Grade 7 Kiswahili Exam Term 3 2026 · Question 13
Andika sifa mbili za Zingo zinazojitokeza katika dondoo hili.
From Kiswahili Paper 2 — October 2026 Collection · 2 marks · Topic: Kusoma, Novela
Mimi nilijisemea kimoyomoyo, “Zingo, lazima uwe jasiri ndiposa uishi vyema. Usiwe legelege.”
Nilijikakamua na kuendelea kusoma riwaya yangu ya Mshale wa Matumaini ili kujipa tumaini. Nilipenda usimulizi wa vitushi vyake vya kusisimua. Lugha yake pia ilikuwa sahili na rahisi kueleweka.
Nilimkumbuka mhusika mkuu alivyokuwa akipitia changamoto nyingi za maisha ili kutimiza ndoto zake za kuwa msanii hodari na wa kutambulika. Mhusika huyu mwanzoni alipuuzwa na kudhaniwa kwamba hakuwa na kipaji chochote cha sanaa. Watu wengi walimsema na kudhihaki juhudi zake lakini hakukata tamaa wala kufa moyo. Hatimaye, mhusika huyo alifanikiwa kuwa miongoni mwa wasanii maarufu duniani.
Wakati nilipochoka kusoma riwaya hiyo, nilisoma Biblia. Niliyapenda mafunzo ya Yusufu, Danieli na Daudi kwenye Biblia. Yalinitia nguvu.
Mama aliamua kuniingiza shuleni pale kambuni. Nilipoingia kidato cha kwanza, shule hiyo iliitwa...

Answer
Zingo ni jasiri kwa sababu anajihimiza asiwe legelege. Pia anapenda kusoma kwa kuwa anasoma riwaya na Biblia.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 7 Kiswahili questions from this test
- Andika aina mbili za mandhari zinazojitokeza katika sehemu hii ya novela.Question 14
- Eleza masuala matatu ambayo yameshughulikiwa katika dondoo hili.Question 15
- Katika dondoo hili, mwandishi ametumia mbinu mbalimbali za lugha kuwasilisha kazi yake. Eleza mbinu mbili alizotumia.Question 16
- Eleza funzo moja unalopata kutokana na tabia ya Zingo.Question 17
- Andika insha ya maelezo kuhusu: BAADA YA DHIKI FARAJA Andika insha yenye maneno kati ya 300 na 350.Question 1
- Je, aina hii ya wimbo huitwaje?Question 2