naQonda

CBC Grade 7 Kiswahili Exam Term 3 2026 · Question 15

Eleza masuala matatu ambayo yameshughulikiwa katika dondoo hili.

From Kiswahili Paper 2 — October 2026 Collection · 3 marks · Topic: Kusoma, Novela

Mimi nilijisemea kimoyomoyo, “Zingo, lazima uwe jasiri ndiposa uishi vyema. Usiwe legelege.”
Nilijikakamua na kuendelea kusoma riwaya yangu ya Mshale wa Matumaini ili kujipa tumaini. Nilipenda usimulizi wa vitushi vyake vya kusisimua. Lugha yake pia ilikuwa sahili na rahisi kueleweka.
Nilimkumbuka mhusika mkuu alivyokuwa akipitia changamoto nyingi za maisha ili kutimiza ndoto zake za kuwa msanii hodari na wa kutambulika. Mhusika huyu mwanzoni alipuuzwa na kudhaniwa kwamba hakuwa na kipaji chochote cha sanaa. Watu wengi walimsema na kudhihaki juhudi zake lakini hakukata tamaa wala kufa moyo. Hatimaye, mhusika huyo alifanikiwa kuwa miongoni mwa wasanii maarufu duniani.
Wakati nilipochoka kusoma riwaya hiyo, nilisoma Biblia. Niliyapenda mafunzo ya Yusufu, Danieli na Daudi kwenye Biblia. Yalinitia nguvu.
Mama aliamua kuniingiza shuleni pale kambuni. Nilipoingia kidato cha kwanza, shule hiyo iliitwa...

Eleza masuala matatu ambayo yameshughulikiwa katika dondoo hili.

Answer

Elimu: Zingo anasoma na kuingia shuleni. Dini: anapata nguvu katika mafunzo ya Biblia. Usanii: mhusika wa riwaya anajitahidi kuwa msanii hodari.

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 7 Kiswahili questions from this test