naQonda

CBC Grade 6 Kiswahili End Term 3 Exam 2026 · Question 1

Safari na Rukia walipatana ukumbini wakati upi?

From Test 1 — Endterm 3 Assessment 2026 (Kiswahili Lugha) · 1 mark · Topic: Kusikiliza na Kuzungumza, Ufahamu wa Mazungumzo

(Safari na Rukia wananyunyuzia mimea maji.)

Safari: Masalkheri, Rukia?
Rukia: Akheri, Safari. Naona umeniwahi kufika leo.
Safari: (Akitabasamu) Nimefika muda mfupi tu uliopita, yapata nusu saa hivi.
Rukia: Nusu saa! Huo ni muda mfupi. Lazima umefaidi maonyesho mengi kabla sijafika.
Safari: Kipendacho moyo ni dawa. Ninayapenda maonyesho ya kitamaduni kwani hunipa fursa ya kipekee ya kujifunza tamaduni za wengine.
Rukia: Huo ni ukweli, ndugu yangu. Isitoshe, tukifurahia tamaduni za wenzetu tutawaelewa zaidi. Hii ni njia ya kuimarisha mshikamano wa kitaifa.
Safari: Naam. Hali kadhalika, mbali na kuiburudisha, uigizaji ni njia mojawapo ya kutambua na kukuza vipawa vyetu.
Rukia: (Akitazama vijana walio jukwani) Hilo linanikumbusha kwamba tulilipa kiingilio ili tupate nafasi hapa ukumbini. Haikosi waigizaji hawa watapata ujira wao kutokana na malipo hayo. Kwa hivyo, tamasha hizo kwa wengine ni njia ya kuumbua riziki.
Safari: Maigizo yenyewe huwa na dhamira mbalimbali, kuna vile kukashifu maovu, kuelimisha na kupinga mila potovu. Bila shaka, hii ni njia mwafaka ya kubadilisha jamii.
Rukia: Naona jukwaa liko tayari sasa. (Anatulia kidogo.) Na ni heri tukae ili tusipitwe na uhondo.
Safari: Sawa, dada yangu.
(Wanatulia kutazama mchezo jukwaani.)

Safari na Rukia walipatana ukumbini wakati upi?

  1. AAsubuhi
  2. BJioni
  3. CAdhuhuri
  4. DUsiku

Answer

B. Jioni

Mazungumzo yanaonyesha kuwa ni jioni (tamasha la jukwaani lililoandaliwa ukumbini huambatana na nyakati za jioni, na muktadha wa mazungumzo unaonyesha hali hii).

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 6 Kiswahili questions from this test