CBC Grade 5 Kiswahili End Term 1 Exam 2025 · Question 4
Paka alikuwa amefunzwa
From Kiswahili — End Term Assessment 2025 (Set 6) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma habari hii kisha ujibu maswali nambari 1-5.
Mwanamke mmoja kwa jina Nuru alikuwa na paka mmoja aliyekuwa maridadi mno. Alimfunza paka huyo mambo mengi, yakiwemo kumlea mtoto. Nuru alikuwa na mtoto mchanga lakini hakuwa na yaya. Hivyo basi siku moja alipotaka kwenda sokoni, alimlaza mtoto kitandani na kumwacha paka hapo ili amchunge. Paka alisonga karibu na mtoto na kutulia akifuata maagizo ya kumlea mtoto.
Baada ya kununua bidhaa mbalimbali, Nuru alirudi nyumbani na jambo la kwanza lilikuwa kwenda kuona kama mtoto wake ameamka. Kabla hajafika kwenye chumba cha mtoto alishangaa. Lo! paka alikuwa pale mlangoni akiwa amejaa damu mdomoni huku akijirambaramba damu kwa furaha. Nuru alikuwa karibu kuzirai.
Alikimbia jikoni akauchukua upanga na kumkatakata paka yule hadi akafa. Kisha alienda chumbani kuona yaliyompata mtoto wake. Hakuamini aliyoona. Mtoto alikuwa pale salama salimini. Chini ya kitanda palikuwa na joka kubwa lililokuwa limeraruliwa kwa makucha ya paka. Kumbe damu iliyokuwa kwenye mdomo wa paka ilikuwa ya joka lile!
4. Paka alikuwa amefunzwa
- Akumlea mtoto
- Bkujiramba midomo
- Ckuwakamata panya
- Dkubaki nyumbani.
Answer
A. kumlea mtoto
"Alimfunza paka huyo mambo mengi, yakiwemo kumlea mtoto."