CBC Grade 5 Kiswahili End Term 1 Exam 2025 · Question 1
Nuru alifanya kitu gani cha kwanza alipofika nyumbani kutoka sokoni?
From Kiswahili — End Term Assessment 2025 (Set 6) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma habari hii kisha ujibu maswali nambari 1-5.
Mwanamke mmoja kwa jina Nuru alikuwa na paka mmoja aliyekuwa maridadi mno. Alimfunza paka huyo mambo mengi, yakiwemo kumlea mtoto. Nuru alikuwa na mtoto mchanga lakini hakuwa na yaya. Hivyo basi siku moja alipotaka kwenda sokoni, alimlaza mtoto kitandani na kumwacha paka hapo ili amchunge. Paka alisonga karibu na mtoto na kutulia akifuata maagizo ya kumlea mtoto.
Baada ya kununua bidhaa mbalimbali, Nuru alirudi nyumbani na jambo la kwanza lilikuwa kwenda kuona kama mtoto wake ameamka. Kabla hajafika kwenye chumba cha mtoto alishangaa. Lo! paka alikuwa pale mlangoni akiwa amejaa damu mdomoni huku akijirambaramba damu kwa furaha. Nuru alikuwa karibu kuzirai.
Alikimbia jikoni akauchukua upanga na kumkatakata paka yule hadi akafa. Kisha alienda chumbani kuona yaliyompata mtoto wake. Hakuamini aliyoona. Mtoto alikuwa pale salama salimini. Chini ya kitanda palikuwa na joka kubwa lililokuwa limeraruliwa kwa makucha ya paka. Kumbe damu iliyokuwa kwenye mdomo wa paka ilikuwa ya joka lile!
1. Nuru alifanya kitu gani cha kwanza alipofika nyumbani kutoka sokoni?
- AKumwua paka.
- BKuchukua upanga.
- CKumwamsha mtoto.
- DKwenda kumwona mtoto.
Answer
D. Kwenda kumwona mtoto.
"jambo la kwanza lilikuwa kwenda kuona kama mtoto wake ameamka".