CBC Grade 5 Kiswahili Mock Exam 2025 · Question 3
Embe moja ni shilingi ngapi?
From Kiswahili — First Trial Assessment 2025 (Set 1) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma mazungumzo kati ya muuzaji na mnunuzi, kisha jibu swali 1-5.
Muuzaji: Karibu mteja wangu, karibu sana hapa! Kila kitu ni bei nzuri sana.
Mnunuzi: Asante.
Muuzaji: Unataka nini? Angalia vizuri. Kila kitu kipo.
Mnunuzi: Mbona leo hujaleta machungwa?
Muuzaji: Machungwa hayapatikani sana siku hizi. Lakini, tazama vizuri. Kuna vitu vingine na hata matunda mengine yapo; mananasi, maembe na maparachichi.
Mnunuzi: Ninataka maembe matatu, nyanya, sukari kilo tatu na chumvi kilo moja na nusu.
Muuzaji: Sawa. Embe moja ni shilingi mia tano, sukari ni shilingi elfu mbili kwa kila kilo, chumvi kilo ni shilingi mia saba. Fungu moja la nyanya ni shilingi mia tano.
Mnunuzi: Mbona unapandisha bei! Punguza kidogo, huoni kwamba sukari inapatikana siku hizi! Nyanya zina bei rahisi vilevile. Tafadhali, punguza kidogo!
Muuzaji: Sawa. Nyanya unataka mafungu mangapi?
Mnunuzi: Mafungu matatu.
Muuzaji: Wewe ni mteja wangu wa kila siku.
Mnunuzi: Sawa. Na sukari?
Muuzaji: Sukari? Leta nusu basi.
Mnunuzi: Asante sana. Nipimie kila kitu. Pesa hizi hapa.
Muuzaji: Asante sana. Ngoja nikuwekee katika mkoba huu.
Mnunuzi: Sawa. Niwekee. (Muuzaji anamwekea bidhaa kwenye mkoba, kisha anampatia)
Muuzaji: Kila kitu kipo tayari.
Mnunuzi: Asante sana.
Muuzaji: Karibu. Karibu tena.
Mnunuzi: Sawa. Kwaheri.
Muuzaji: Kwaheri ya kuonana.
3. Embe moja ni shilingi ngapi?
- AMia tano.
- BMia moja.
- CLaki mbili.
- DElfu moja.
Answer
A. Mia tano.
"Embe moja ni shilingi mia tano."
More Grade 5 Kiswahili questions from this test
- Chakula kipi kilikuwa bei rahisi?Question 4
- Mnunuzi aliwekewa vitu wapi?Question 5
- Sungura alijulikana kuwaQuestion 6
- Simba alipofika kwa Sungura alipiga hodi. Sungura alimjibu vipi?Question 7
- Simba walihimizwa watakula mzoga wa wanyama wapi?Question 8
- Sungura alimwambia Simba akale wanyama gani?Question 9