naQonda

CBC Grade 5 Kiswahili Mock Exam 2025 · Question 1

Kwa sababu gani muuzaji hana machungwa?

From Kiswahili — First Trial Assessment 2025 (Set 1) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu

Soma mazungumzo kati ya muuzaji na mnunuzi, kisha jibu swali 1-5.
Muuzaji: Karibu mteja wangu, karibu sana hapa! Kila kitu ni bei nzuri sana.
Mnunuzi: Asante.
Muuzaji: Unataka nini? Angalia vizuri. Kila kitu kipo.
Mnunuzi: Mbona leo hujaleta machungwa?
Muuzaji: Machungwa hayapatikani sana siku hizi. Lakini, tazama vizuri. Kuna vitu vingine na hata matunda mengine yapo; mananasi, maembe na maparachichi.
Mnunuzi: Ninataka maembe matatu, nyanya, sukari kilo tatu na chumvi kilo moja na nusu.
Muuzaji: Sawa. Embe moja ni shilingi mia tano, sukari ni shilingi elfu mbili kwa kila kilo, chumvi kilo ni shilingi mia saba. Fungu moja la nyanya ni shilingi mia tano.
Mnunuzi: Mbona unapandisha bei! Punguza kidogo, huoni kwamba sukari inapatikana siku hizi! Nyanya zina bei rahisi vilevile. Tafadhali, punguza kidogo!
Muuzaji: Sawa. Nyanya unataka mafungu mangapi?
Mnunuzi: Mafungu matatu.
Muuzaji: Wewe ni mteja wangu wa kila siku.
Mnunuzi: Sawa. Na sukari?
Muuzaji: Sukari? Leta nusu basi.
Mnunuzi: Asante sana. Nipimie kila kitu. Pesa hizi hapa.
Muuzaji: Asante sana. Ngoja nikuwekee katika mkoba huu.
Mnunuzi: Sawa. Niwekee. (Muuzaji anamwekea bidhaa kwenye mkoba, kisha anampatia)
Muuzaji: Kila kitu kipo tayari.
Mnunuzi: Asante sana.
Muuzaji: Karibu. Karibu tena.
Mnunuzi: Sawa. Kwaheri.
Muuzaji: Kwaheri ya kuonana.

1. Kwa sababu gani muuzaji hana machungwa?

  1. AYalikuwa yameoza.
  2. BHaikuwa msimu wa machungwa.
  3. CAlikosa pesa za kununua.
  4. DAlikuwa amechelewa kuchukua sokoni.

Answer

B. Haikuwa msimu wa machungwa.

Muuzaji anasema "Machungwa hayapatikani sana siku hizi": si msimu wake.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 5 Kiswahili questions from this test