CBC Grade 5 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 4
Inaonekana Zawadi na Lydia ni
From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 5) · 1 mark · Topic: Kusoma, Mazungumzo
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali yatakayofuata.
(Zawadi na Lydia wanakutana. Mazungumzo yao yanakuwa hivi.)
Zawadi: Masalkheri Lydia.
Lydia: Akheri Zawadi. Naona umewahi kufika leo.
Zawadi: (Akitabasamu) Nimefika muda mfupi tu uliopita yapata nusu saa hivi.
Lydia: Nusu saa! Huo si muda mfupi. Lazima umefaidi maonyesho mengi kabla sijafika.
Zawadi: Kipendacho moyo ni dawa. Ninayapenda maonyesho ya kitamaduni kwani hunipa fursa ya kipekee ya kujifunza tamaduni za wengine.
Lydia: Hayo ni kweli ndugu yangu. Isitoshe, tukifurahia tamaduni za wenzetu, tutaelewa zaidi. Hii ni njia muhimu ya kuimarisha mshikamano wa kitaifa.
Zawadi: Naam, hali kadhalika, uigizaji ni njia mojawapo ya kutambua na kukuza vipawa vyetu.
Lydia: (Akiwatazama vijana walio jukwaani) Hilo linanikumbusha kwamba tulilipa kiingilio ili tupate nafasi hapa ukumbini. Haikosi waigizaji hawa watapata ujira wao kutokana na malipo hayo. Kwa hivyo tamasha hizi kwa wengine ni njia ya kupata riziki.
Zawadi: Maagizo yenyewe huwa na malengo ya kuonyadhihidi ya maovu katika jamii, kuelimisha na kupinga mila mbovu.
Lydia: Naona jukwaa li tayari sasa. (Anatua kidogo) Ni heri tutulie ili tusipitwe na uhondo.
Zawadi: Sawa dada yangu. (Wanatulia kutazama mchezo jukwaani)
4. Inaonekana Zawadi na Lydia ni
- Andugu
- Bmaadui
- Cwaigizaji
- Dmarafiki
Answer
D. marafiki
Wanazungumza kwa urafiki.
More Grade 5 Kiswahili questions from this test
- Zawadi na Lydia walienda kutazama maonyesho wapi?Question 5
- Ni nani aliyekuwa na wazo la kukabiliana na uhalifu katika kijiji hicho?Question 6
- Busara alifanya nini kwa vijana waliokuwa wakijaribu kutekeleza wizi?Question 7
- Kwa nini vijana walijuta baada ya mazungumzo na Busara?Question 8
- Kwa upande wa jamii nini kilitokea baada ya vijana kuachana na uhalifu?Question 9
- Ni nini kinachohitajika ili kufikia afya bora?Question 10