naQonda

CBC Grade 4 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 1

Kwa nini Bi. Nia alisisitiza mavazi safi na yenye staha shuleni?

From Kiswahili — Revision Paper 6 (2026) · 1 mark · Topic: Kusikiliza na Kuzungumza, Ufahamu wa Mazungumzo

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 1-5.

Maria: Shikamoo mwalimu?
Bi. Nia: Marahaba Maria, unaendeleaje?
Maria: Vyema. Ningependa kujua ni mavazi gani yanayofaa kuvaliwa shuleni.
Bi. Nia: Ni vizuri kuvaa mavazi safi na yenye staha. Kwa mfano, shati safi na suruali au sketi isiyo fupi sana.
Maria: Je, viatu navyo vina umuhimu?
Bi. Nia: Ndio, viatu safi na vilivyofungwa ni bora zaidi shuleni. Hii huonyesha nidhamu na heshima.
Maria: Nashukuru kwa maelezo Bi. Nia. Nitayazingatia.
Bi. Nia: Vizuri sana Maria. Endelea kuwa na nidhamu na muonekano mzuri.
Maria: Asante sana Bi. Nia. Kwaheri.
Bi. Nia: Kwaheri Maria, nakutakia siku njema.

Kwa nini Bi. Nia alisisitiza mavazi safi na yenye staha shuleni?

  1. AIli kuonyesha urembo wa mwanafunzi.
  2. BIli kuonyesha nidhamu na heshima.
  3. CIli kushindana na wanafunzi wengine.
  4. DIli kufuata mitindo ya kisasa.

Answer

B. Ili kuonyesha nidhamu na heshima.

Bi. Nia anasema mavazi safi na viatu vilivyofungwa "huonyesha nidhamu na heshima".

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 4 Kiswahili questions from this test