CBC Grade 4 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 5
Kwanini Maria alihitimisha mazungumzo kwa kusema "kwaheri" badala ya kuondoka kimya kimya?
From Kiswahili — Revision Paper 6 (2026) · 1 mark · Topic: Kusikiliza na Kuzungumza, Ufahamu wa Mazungumzo
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 1-5.
Maria: Shikamoo mwalimu?
Bi. Nia: Marahaba Maria, unaendeleaje?
Maria: Vyema. Ningependa kujua ni mavazi gani yanayofaa kuvaliwa shuleni.
Bi. Nia: Ni vizuri kuvaa mavazi safi na yenye staha. Kwa mfano, shati safi na suruali au sketi isiyo fupi sana.
Maria: Je, viatu navyo vina umuhimu?
Bi. Nia: Ndio, viatu safi na vilivyofungwa ni bora zaidi shuleni. Hii huonyesha nidhamu na heshima.
Maria: Nashukuru kwa maelezo Bi. Nia. Nitayazingatia.
Bi. Nia: Vizuri sana Maria. Endelea kuwa na nidhamu na muonekano mzuri.
Maria: Asante sana Bi. Nia. Kwaheri.
Bi. Nia: Kwaheri Maria, nakutakia siku njema.
Kwanini Maria alihitimisha mazungumzo kwa kusema "kwaheri" badala ya kuondoka kimya kimya?
- AIli kuonyesha furaha yake.
- BIli kuonyesha heshima na adabu.
- CIli kuomba ruhusa ya kuondoka.
- DIli kuonyesha hasira yake.
Answer
B. Ili kuonyesha heshima na adabu.
Kuaga kwa kusema "kwaheri" ni adabu njema; kunaonyesha heshima kwa mtu uliyekuwa ukizungumza naye.
More Grade 4 Kiswahili questions from this test
- Bendera ya Kenya ilipitishwa rasmi mwaka waQuestion 6
- Rangi nyekundu kwenye bendera ya Kenya inawakilisha nini?Question 7
- Bendera ya Kenya ina rangi ngapi kwa jumla?Question 8
- Rangi ya kijani kwenye bendera inawakilisha nini?Question 9
- Miembe hutupatia matunda gani?Question 10
- Michungwa ni muhimu kwa sababu gani?Question 11