CBC Grade 4 Kiswahili Exam Term 2 2025 · Question 1
Ndege wa kwanza kumshauri kiboko alikuwa nani?
From Kiswahili — CBC Assessment 2025 (Set 6) (Lugha) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Hadithi
Soma hadithi ifuatayo kisha ujibu swali la 6 - 10.
Hapo zamani Kiboko alitaka kujua wakati ambao angeacha kula na kwenda kujificha majini. Basi rafiki yake Mamba akamwambia awaulize ndege fulani ambao wangeweza kumjulisha saa.
Ndege wa kwanza kumshauri alikuwa Gude ambaye alimwambia, "Ukinisikia nikilia dwi! dwi! du! du! acha kula mara moja, ukimbie uende ukajifiche." Usiku uliofuata yule Gude alilia mapema sana na Kiboko akafanya kama alivyoambiwa. Lakini alikaa kwa muda mrefu sana bila kupambazuka, kwa hivyo akarudi tena.
Siku ya pili, Kiboko alimwendea ndege anayeitwa Mlamba kutaka ushauri wa kuacha kula. Alimwambia wakati angemsikia Mlamba akilia kucha! kucha! aache kula na kurudi majini. Usiku huo Mlamba alichelea kulia kwa hivyo Kiboko alichelewa kurudi majini.
Kabla hajakata tamaa, Kiboko alimwendea Jogoo. Jogoo akamshauri, "Nitawika mara mbili 'kaliki kuuu! kuuu! kalikikuu!' na nikiwika mara ya tatu huna budi kurudi majini." Kiboko alifuata mashauri ya jogoo na mpaka leo Kiboko hajachelewa tena kurudi majini.
6. Ndege wa kwanza kumshauri kiboko alikuwa nani?
- AMlamba
- BGude
- CMamba
- DJogoo.
Answer
B. Gude
"Ndege wa kwanza kumshauri alikuwa Gude."