CBC Grade 3 Kiswahili Opener Exam Term 3 2026 · Question 13
Watoto hawa wanasoma darasa gani?
From Kiswahili — Term 3 Opener Exams 2026 · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Ufahamu 2
Soma kisa hiki kisha ujibu maswali.
Nuru na Natia ni marafiki. Wanasoma darasa la tatu katika shule ya msingi ya Malinya. Marafiki hawa mara nyingi hutembeleana nyumbani. Siku moja Nuru aliamua kumtembelea Natia nyumbani kwao. Alimkuta mama yake Natia akiwa amelala barazani. Siku hiyo Natia hakuwa nyumbani. Alimsogelea na kumwamkua mama yake Natia.
Mama yake Natia alimweleza Nuru kuwa alikuwa anaumwa sana. Nuru alimpa pole. Mara alienda kutafuta msaada kwa majirani. Majirani wawili walifika na kumpeleka mama yake Natia hospitalini. Alipofika hospitalini, daktari alimtibu na kuruhusiwa kurudi nyumbani. Natia alifurahia aliporudi nyumbani. Alimshukuru Nuru kwa upendo aliouonyesha kwa mama yake.
2. Watoto hawa wanasoma darasa gani?
Answer
darasa la tatu
Kisa kinasema: darasa la tatu.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 3 Kiswahili questions from this test
- Nuru alimkuta mama yake Natia akiwa amelala wapi?Question 14
- Nani walimsaidia Nuru kumpeleka mama yake Natia hospitalini?Question 15
- Mama yake Natia alipofika hospitalini alihudumiwa na nani?Question 16
- SEHEMU YA 4: SARUFI Soma kisha ujaze nafasi kwa kutumia maneno uliyopewa. (a)Question 17
- Tunga sentensi ukitumia vifaa hivi vya shambani. a)Question 22
- Andika sentensi hizi kwa umoja a) Wao wataimba keshoQuestion 25