CBC Grade 9 Kiswahili Revision Exam · Question 1
Kila sikuya Dominika Jamila alifanyanini?
From Test 95 — Revision 1 Kiswahili Karatasi 1 · 1 mark · Topic: Kusoma, Kusoma kwa Ufahamu
Kifungu cha Maswali 1–6
Jamila alikuwa mwanamke mwenye bidii mithili ya mchwa. Kila siku ya Dominika Jamila aliamka
asubuhi na mapema ili kufanya usafi wa nyumba. Hii ndiyo siku ambayo alisafisha kila sehemu ya nyumba,
kutoa vumbi kwenye vifaa vyake, kutoa utando kwenye kuta na kunadhifisha chumba cha kuku wake. Bwana
Musa, mume wake, alienda shambani kutafutamajani ya kuliwa na mifugo wao. Mtoto wao ambaye alikuwa
na umri wa miaka mitano alikaa na bibi na kurejeshwa kwao wikendi.
Mara tu baada ya kukamilisha kula kiamshakinywa, Jamila alichukua ndoo ndogo mbili. Moja alitia
maji yenye sabuni na nyingine maji safi yasiyo na sabuni. Alitia vitambaa viwili ndani yake. Alianza kwa
kupangusa meza, viti na kabati. Baadaye alipangusa vioo vya madirisha na milango yote. Kila alipotumia
maji yenye sabuni, alirudia kwa mara ya pili na maji yasiyo na sabuni ili kuhakikisha sehemu hiyo imeng'aa.
Baada ya kumaliza kupangusa sehemy hizo, alichukua ndoo kubwa na taulo kuukuu. Alipiga deki sakafu
yote huku akisafisha hadi mvunguni mwa makochi na vitanda. Alifanyä hivyo ili kuzuia magonjwa yaletwayo
na vumbi nyumbani kama vile mafua.ÄAlipokamilisha kusafisha nyumba, alifululiza hadi kwenye chumba
chakuku na kuwafungulia kuku wake ili äfagie. Alifagia na kunyunyizia dawa ya kuzuia funza kuwavamia
kuku wake. Vilevile, alisafisha vyombo vyao vya chakula. Alivisafisha vyombo hivi kila siku ili kuzuia
magonjwa ya kuku
Kwa kuhitimisha, Jamila alifagia nje ya nyumba na kuchoma taka za wiki nzima katika eneo lililotengewa
kazi hiyo. Mume wake alipowasili alilengeta ua uliozunguka boma Iao ili kuzuia mbu wasiwavamie. Baadaye,
Jamila aliandaa chamcha na wote wakala wakifurahia mazingira safi.

- AKulengeta ua uliozunguka boma
- BKufanya usafi nyumbani kwao
- CKutafuta majam ya mifugo wao,
- DKwenda kwa bibi kumchukua mwana wao
Answer
B. Kufanya usafi nyumbani kwao
The correct option is B.
More Grade 9 Kiswahili questions from this test
- Je, nikazi ganikati ya hizihaikufanywanaJamila siku ya Jumapili?Question 2
- Je, unadhani ni nini kingetokea iwapo Jamila hangefanya usafi wa nyumbani?Question 3
- Ni jibu lipi linaloonyesha mfuatano ufaao wa matendo ambayo Jamila alifanya kila siku ya Dominika?Question 4
- Kauli ‘piga deki’ ni mbinu gani ya lugha?Question 5
- Uchafu wa vumbi husababisha ugonjwa waQuestion 6
- Kulingana na aya ya kwanza, Paka alitoa wapi shamba waliloishi na Panya?Question 7