naQonda

CBC Grade 9 Kiswahili Revision Exam · Question 4

Ni jibu lipi linaloonyesha mfuatano ufaao wa matendo ambayo Jamila alifanya kila siku ya Dominika?

From Test 95 — Revision 1 Kiswahili Karatasi 1 · 1 mark · Topic: Kusoma, Kusoma kwa Ufahamu

Kifungu cha Maswali 1–6
Jamila alikuwa mwanamke mwenye bidii mithili ya mchwa. Kila siku ya Dominika Jamila aliamka
asubuhi na mapema ili kufanya usafi wa nyumba. Hii ndiyo siku ambayo alisafisha kila sehemu ya nyumba,
kutoa vumbi kwenye vifaa vyake, kutoa utando kwenye kuta na kunadhifisha chumba cha kuku wake. Bwana
Musa, mume wake, alienda shambani kutafutamajani ya kuliwa na mifugo wao. Mtoto wao ambaye alikuwa
na umri wa miaka mitano alikaa na bibi na kurejeshwa kwao wikendi.
Mara tu baada ya kukamilisha kula kiamshakinywa, Jamila alichukua ndoo ndogo mbili. Moja alitia
maji yenye sabuni na nyingine maji safi yasiyo na sabuni. Alitia vitambaa viwili ndani yake. Alianza kwa
kupangusa meza, viti na kabati. Baadaye alipangusa vioo vya madirisha na milango yote. Kila alipotumia
maji yenye sabuni, alirudia kwa mara ya pili na maji yasiyo na sabuni ili kuhakikisha sehemu hiyo imeng'aa.
Baada ya kumaliza kupangusa sehemy hizo, alichukua ndoo kubwa na taulo kuukuu. Alipiga deki sakafu
yote huku akisafisha hadi mvunguni mwa makochi na vitanda. Alifanyä hivyo ili kuzuia magonjwa yaletwayo
na vumbi nyumbani kama vile mafua.ÄAlipokamilisha kusafisha nyumba, alifululiza hadi kwenye chumba
chakuku na kuwafungulia kuku wake ili äfagie. Alifagia na kunyunyizia dawa ya kuzuia funza kuwavamia
kuku wake. Vilevile, alisafisha vyombo vyao vya chakula. Alivisafisha vyombo hivi kila siku ili kuzuia
magonjwa ya kuku
Kwa kuhitimisha, Jamila alifagia nje ya nyumba na kuchoma taka za wiki nzima katika eneo lililotengewa
kazi hiyo. Mume wake alipowasili alilengeta ua uliozunguka boma Iao ili kuzuia mbu wasiwavamie. Baadaye,
Jamila aliandaa chamcha na wote wakala wakifurahia mazingira safi.

Ni jibu lipi linaloonyesha mfuatano ufaao wa matendo ambayo Jamila alifanya kila siku ya Dominika?

  1. AKufuta vumbi, kutafuta majani na kuandaa chamcha.
  2. BKufagia chumba cha kuku, kufyeka nyasi, kupiga deki na kuandaa chamcha.
  3. CKupiga deki, kupangusa vumbi, kuandaa chamcha na kufagia chumba cha kuku.
  4. DKufuta vumbi, kupiga deki, kufagia chumba cha kuku na kuandaa chamcha.

Answer

D. Kufuta vumbi, kupiga deki, kufagia chumba cha kuku na kuandaa chamcha.

The correct option is D.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 9 Kiswahili questions from this test