naQonda

CBC Grade 9 Kiswahili Exam Term 2 2026 · Question 8

Chagua methali ifaayo zaidi kujumuisha ujumbe wa hadithi hii.

From Test 92 — Kiswahili Karatasi 1 Muhula 2 Mei 2026 · 1 mark · Topic: Fasihi, Fasihi Simulizi

Source text
Hapo zamani za kale, katika nchi ya Nuru, paliishi kijana aliyeitwa Mwamba. Kijana huyo alienziwa sana na wakazi wengine kutokana na nguvu na jitihada zake za kuitetea jamii yake. Wakazi wengi walitegemea kilimo cha mimea na ufugaji wa wanyama. Mara kwa mara, mahasidi zao waliwavamia kwa azma ya kuiba mifugo lakini kila walipofika, Mwamba aliwaongoza mashujaa wenzake wakawasukuma maadui wale hadi nje ya mipaka yao. Wale waliodiriki kuonyesha ukaidi waliangushwa na upanga wa Mwamba.
Miaka ilizidi kusonga hata ukafika wakati wa Mwamba kupata jiko. Alitafutiwa mabinti wote warembo kutoka jamii yake lakini akakataa katakata kuwaoa. Alisema kwamba anataka mke katika nchi ya mbali.
Wazee wake walimpa radhi zao akafunga safari asubuhi moja.
Baada ya kupiga milundi kwa juma zima, Mwamba alijipata katika nchi ya Mavuno. Wenyeji wa huko walikuwa waja wakarimu na wenye mioyo safi. Mwamba alipokelewa kwa mikono miwili na kila familia aliyoitembelea. Mabinti wa huko walikuwa hurulaini. Haukupita muda, Mwamba akampata mmoja aliyempendeza akaamua kumwoa.
Utamaduni wa Mavuno ulimhitaji mtu amsaidie baba mkwe katika kazi zake kwa mwezi mmoja kabla ya kukabidhiwa mke. Baada ya hapo, mtu na mchumba wake wangepelekwa mbele ya baraza la wazee wafanyiwe tambiko ili kuwakinga dhidi ya mikosi ya aina yoyote. Mwamba alipoarifiwa hayo, alicheka hadi mbavu zikavunjika. Alidai kwamba yeye alikuwa radhi kulipa kiasi chochote cha mahari almradi asishiriki utamaduni wowote wa kishenzi. Juhudi za kumrai asipuuze kaida hizo ziliambulia patupu.
Mwishowe wazee wakaamua kuwa, mtoto akililia wembe mpe.
Mwamba alimchukua mchumba wake bila baraza za wazee akashika tariki kurudi nyumbani. Moyoni aliona fahari kwa ushindi wake. Njiani alikuwa akiimba nyimbo ambazo kwa kawaida waliimba na wenzake kila walipopata ushindi dhidi ya mahasimu.
Ghafla bin vuu, walizuka mashujaa waliojihami wakamkabili Mwamba ana kwa ana. Mwamba ni nani?
Alipambana nao kiume. Aliwaangamiza wavamizi wale takriban wote. Hata hivyo, alikuwa ameumia vibaya. Wale waliosalia walimchukua mchumba wake wakatoroka. Mwamba alibaki akiuguza majeraha ya mwili na roho.
Laiti Mwamba angalisikiza rai ya wazee hayo yasingalimfika. Mbali na kupokea baraka za wazee, angepewa vijana wa kumsindikiza hadi kwao. Aliwaza hayo yote moyoni lakini akajua kuwa maji yakimwagika hayazoleki.

Chagua methali ifaayo zaidi kujumuisha ujumbe wa hadithi hii.

  1. AKwa mwoga huenda kicheko kwa shujaa huenda kilio.
  2. BBaada ya dhiki ni faraja.
  3. CMwenye nguvu mpishe.
  4. DMajuto ni mjukuu huja baadaye.

Answer

B. Baada ya dhiki ni faraja.

The correct option is B: Baada ya dhiki ni faraja.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 9 Kiswahili questions from this test