naQonda

CBC Grade 9 Kiswahili Exam Term 2 2026 · Question 13

Kulingana na kifungu, eneo lenye misitu

From Test 92 — Kiswahili Karatasi 1 Muhula 2 Mei 2026 · 1 mark · Topic: Kusoma, Kusoma kwa Ufahamu

Source text
Maliasili ni vitu vyote vinavyotokana na maumbile kama vile madini, misitu, wanyamapori, bahari, mito na maziwa ambayo hupatikana katika mazingira yetu. Japo binadamu mwenyewe hakuhusika katika kuumba maliasili, hana budi kuzitunza na hata kuongeza thamani pale awezapo. Hata hivyo, inasikitisha kumwona binadamu yuyo huyo, kwa kuongozwa na tamaa iliyokithiri, akiziharibu maliasili kiholela.
Misitu ni maliasili muhimu. Ni ukweli usiopingika kuwa misitu ndiyo huchangia katika kuvuta mvua. Mahali palipo na misitu hupata mvua inayotegemewa msimu baada ya msimu. Ni muhali kwa wakazi wa mahali kama hapo kushindwa kujitosheleza kwa chakula. Mbali na hayo, misitu ni makazi ya wanyama na ndege mbalimbali. Kuna watu ambao huikata mti katika misitu kiholela kwa tamaa ya kutajirika upesi kwa kuuza mbao au kuchoma makaa. Huko ni kujipalia makaa. Tunapaswa kuitunza misitu ili tusikaushe vyanzo vya maji. Aidha, tuendelee kupanda miti ya kiasili na ya kisasa katika misitu ili tujivunie manufaa ambayo ni tumbi nzima.
Mito, maziwa na bahari ni maliasili muhimu sana nchini. Biashara ya uvuvi huendeshewa humo. Bila shaka, ni vitegauchumi muhimu kwa wavuvi wengi. Isitoshe, maji yanayopatikana humo hutumiwa katika shughuli za nyumbani, zaraa na hata viwandani.
Mara nyingi maji ya mito huchafuliwa kwa kemikali zenye sumu kutoka nyumbani, mashambani, viwandani na kwingineko. Matokeo yake huwa vifo vya wanyama mbalimbali wa majini. Meli zinazosafirisha mafuta, shughuli za kujistarehesha na mabadiliko ya tabia-nchi ni tishio kwa mito, maziwa na bahari zetu. Ni vyema kukomesha vitendo vinavyoharibu maji yetu tusije kuathirika. Tukumbuke kuwa msiba wa kujitakia hauna kilio.
Jukumu la kutunza maliasili ni la kila mwananchi. Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu. Tuungane kupanda miti kwa wingi. Tufanye bega kwa bega shughuli za usafi katika kingo za mito, fuo za bahari na maziwa yetu. Tuwatunze Wanyama wetu na kuwashtaki majangili ili wafunguliwe mashtaka. Kwa vyovyote vile, tusijipakatie mikono na kudai kuwa huo ni wajibu wa serikali.

Kulingana na kifungu, eneo lenye misitu

  1. Ahupata mvua wakati wote
  2. Bhuwa na mazingira bora ya kilimo
  3. Chuwa na uhaba wa chakula
  4. Dhalina shughuli nyingi za kiuchumi.

Answer

B. huwa na mazingira bora ya kilimo

The correct option is B: huwa na mazingira bora ya kilimo.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 9 Kiswahili questions from this test