naQonda

CBC Grade 9 Kiswahili Exam Term 2 2026 · Question 24

Mazungumzo haya yalikuwa na wahusika wangapi?

From Test 92 — Kiswahili Karatasi 1 Muhula 2 Mei 2026 · 1 mark · Topic: Kusikiliza na Kuzungumza, Mazungumzo na Uzungumzaji

Source text
(Babu ameketi na wajukuu wake chini ya mti)
Vijana: Shikamoo babu?
Babu: Marahaba wajukuu wangu. Nimefurahi sana kwa kuwaona.
Halima: Nasi tumefurahi pia babu. Siku zote sisi hufurahia kusikiliza ngano zako tamutamu zilizojaa mafunzo.
Babu: (Akizima redio aliyokuwa akisikiliza) Mwajua nimesikia habari za kuatua moyo kwenye redio. Habari zenyewe zimeniacha na huzuni tele.
Boru: Habari zipi babu? Wajua siku hizi dunia imejaa vituko.
Babu: Taarifa zenyewe ni kuhusu kijana aliyejaribu kujitia kitanzi.
Vijana: (Wakionyesha mshtuko) Lo!
Bela: Siku hizi vijana wengi wana matatizo ya kikatili. Japo wanaonekana wazima barabarani, wengi wao wana msongo wa mawazo.
Halima: Naam, tulijadili hayo darasani. Wapo vijana wanaoathiriwa na mihadarati wengine nao, kwa kuengwaengwa na wazazi na walezi wao wanashindwa kukabiliana na changamoto za maisha.
Bela: Babu, nyinyi mlipokuwa vijana hakukuwa na matukio kama haya?
Babu: Kama yalikuweko, basi yalikuwa machache sana. Siku hizo, tulijitenga na dawa za kulevya. Pia, tulitafuta ushauri wa wakubwa wetu tulipokabiliwa na changamoto. Siku zote tulikumbuka kuwa jungu kuu halikosi ukoko.
Boru: Hata sasa tunaweza kuyaepuka mambo kama hayo. Kupita ushauri wa marika, tunaweza kuelimishana na kutiana moyo bila kupotoshana.
Babu: Kesho tutaongea kuhusu njia za kuimarisha afya ya akili. Nitawasimulia kisa cha kuvutia. Kwa sasa naomba tuingie nyumbani tusije tukazizima kwa baridi. (Halima anambebea babu kibago)

Mazungumzo haya yalikuwa na wahusika wangapi?

  1. AWanne
  2. BWatatu
  3. CKumi na wawili
  4. DWatano

Answer

A. Wanne

The correct option is A: Wanne.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 9 Kiswahili questions from this test