naQonda

CBC Grade 9 Kiswahili Opener Exam Term 1 2025 · Question 34

Bibi yako amekusimulia hadithi hii. Andika funzo moja utakalopata.

From Test 121 — Kiswahili Mukula wa 1 2025 · 1 mark · Topic: Fasihi, Fasihi Simulizi

Soma/Read the source text, then answer.
Hapo zamani za kale, palikuwa na sungura na mamba. Sungura alikuwa mfanyabiashara mashuhuri. Kila siku ya Jumamosi, alikuwa akivuka ng’ambo ya ziwa kuenda kununua bidhaa katika soko lililokuwa katika ng’ambo ya pili.

Kila mara alipofika kando ya ziwa, alikuwa akimpata mamba ambaye alimvusha hadi ng’ambo ya pili. Hata aliporejea na bidhaa zake, mamba alimvusha yeye na bidhaa hizo bila kusita. Kwa upande wake, sungura alimletea mamba matunda ili kuonyesha shukrani kwake.

Siku moja, sungura alinunua bidhaa nyingi kupindukia. Bila shaka alitamani kupata faida kubwa. Aliwalipa wapagazi wakazibeba bidhaa hizo hadi ufuoni. Alimkuta rafiki yake akimsubiri kama kawaida. Mamba alipozitazama bidhaa hizo, aliona kuwa ingekuwa vigumu kuvisomba pamoja na sungura. Alipendekeza apeleke bidhaa kwanza ndipo amrudie sungura. Pendekezo hilo lilimghadhabisha sungura. Alizua madai kwamba mamba alikuwa na njama za kumwibia bidhaa zake.

“Hivi wewe huna shukrani? Siku zote nimekuwa nikikulipa vizuri ili unihudumie. Hivi leo unadiriki kuzimezea mate bidhaa zangu? Wewe na fisi hamna tofauti,” alifoka sungura kwa ghadhabu.

Mamba alipigwa na butwaa. Kumbe siku zote sungura aliona anamlipa ilhali yeye alichukulia kuwa anapalilia urafiki wao. Mamba alijibu kwa upole. “Basi kama ni hivyo, ukimpa mtu kazi pataneni ujira. Mimi najiuzulu kazi hii. Mtafute mwingine akufanyie kazi.” Baada ya hapo mamba aliogelea polepole hadi upande wa pili wa ziwa.

Wanyama wa majini waliposikia yaliyomfika mamba, waliapa kwamba katu wasingemsaidia sungura ambaye hakuwa na shukrani. Sungura alisema kwa kejeli, “Si lazima niogelee. Ninaweza kulizunguka ziwa bila msaada wenu.”

Sungura alifunga safari na bidhaa zake. Safari ambayo ingemchukua siku mbili ilichukua jumla ya siku saba. Bidhaa nyingi ziliharibika. Alipata hasara kubwa kutokana na kiburi chake. Alijuta kwa maneno aliyomwambia mamba lakini maji yakimwagika hayazoleki.

Bibi yako amekusimulia hadithi hii. Andika funzo moja utakalopata.

Answer

Tunapaswa kuwa na shukrani na kuwaheshimu wanaotusaidia.

A complete answer could be: Tunapaswa kuwa na shukrani na kuwaheshimu wanaotusaidia.

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 9 Kiswahili questions from this test