CBC Grade 9 Kiswahili Opener Exam Term 1 2025 · Question 29
Andika sifa tatu za hadithi za aina hii.
From Test 121 — Kiswahili Mukula wa 1 2025 · 3 marks · Topic: Fasihi, Fasihi Simulizi
Soma/Read the source text, then answer.
Hapo zamani za kale, palikuwa na sungura na mamba. Sungura alikuwa mfanyabiashara mashuhuri. Kila siku ya Jumamosi, alikuwa akivuka ng’ambo ya ziwa kuenda kununua bidhaa katika soko lililokuwa katika ng’ambo ya pili.
Kila mara alipofika kando ya ziwa, alikuwa akimpata mamba ambaye alimvusha hadi ng’ambo ya pili. Hata aliporejea na bidhaa zake, mamba alimvusha yeye na bidhaa hizo bila kusita. Kwa upande wake, sungura alimletea mamba matunda ili kuonyesha shukrani kwake.
Siku moja, sungura alinunua bidhaa nyingi kupindukia. Bila shaka alitamani kupata faida kubwa. Aliwalipa wapagazi wakazibeba bidhaa hizo hadi ufuoni. Alimkuta rafiki yake akimsubiri kama kawaida. Mamba alipozitazama bidhaa hizo, aliona kuwa ingekuwa vigumu kuvisomba pamoja na sungura. Alipendekeza apeleke bidhaa kwanza ndipo amrudie sungura. Pendekezo hilo lilimghadhabisha sungura. Alizua madai kwamba mamba alikuwa na njama za kumwibia bidhaa zake.
“Hivi wewe huna shukrani? Siku zote nimekuwa nikikulipa vizuri ili unihudumie. Hivi leo unadiriki kuzimezea mate bidhaa zangu? Wewe na fisi hamna tofauti,” alifoka sungura kwa ghadhabu.
Mamba alipigwa na butwaa. Kumbe siku zote sungura aliona anamlipa ilhali yeye alichukulia kuwa anapalilia urafiki wao. Mamba alijibu kwa upole. “Basi kama ni hivyo, ukimpa mtu kazi pataneni ujira. Mimi najiuzulu kazi hii. Mtafute mwingine akufanyie kazi.” Baada ya hapo mamba aliogelea polepole hadi upande wa pili wa ziwa.
Wanyama wa majini waliposikia yaliyomfika mamba, waliapa kwamba katu wasingemsaidia sungura ambaye hakuwa na shukrani. Sungura alisema kwa kejeli, “Si lazima niogelee. Ninaweza kulizunguka ziwa bila msaada wenu.”
Sungura alifunga safari na bidhaa zake. Safari ambayo ingemchukua siku mbili ilichukua jumla ya siku saba. Bidhaa nyingi ziliharibika. Alipata hasara kubwa kutokana na kiburi chake. Alijuta kwa maneno aliyomwambia mamba lakini maji yakimwagika hayazoleki.

Answer
Wahusika ni wanyama; wanyama hupewa sifa na matendo ya binadamu; hadithi hufundisha maadili au funzo.
A complete answer could be: Wahusika ni wanyama; wanyama hupewa sifa na matendo ya binadamu; hadithi hufundisha maadili au funzo.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 9 Kiswahili questions from this test
- Taja wahusika wawili katika hadithi hii.Question 30
- Ni shughuli ipi ya kiuchumi aliyoshiriki sungura?Question 31
- Iwapo ungekutana na sungura, ungempa ushauri gani?Question 32
- Ni jambo lipi linaloonyesha kuwa wanyama waliamua kumrekebisha sungura?Question 33
- Bibi yako amekusimulia hadithi hii. Andika funzo moja utakalopata.Question 34
- Ni mandhari yapi yanayojitokeza katika dondoo hili?Question 35