naQonda

CBC Grade 6 Kiswahili End Term 2 Exam 2026 · Question 1

Andika jibu sahihi la salamu aliyopewa Mapunda na Chifu.

From Test 6 — Term 2: Endterm Assessment 2026 (Kiswahili Lugha) · 1 mark · Topic: Kusikiliza na Kuzungumza, Ufahamu wa Mazungumzo

Mazungumzo kati ya Chifu na Mapunda
(Mapunda amefikishwa kwa Chifu akiwa amefungwa mikononi kwa kosa la wizi. Ni asubuhi na kikundi cha watu kimeketi nje ya ofisi ya Chifu.)
Chifu: Hujambo Mapunda? Mbona unaonekana na wasiwasi?
Mapunda: (Kwa woga) Mimi ni mzima na sina wasiwasi, Bwana Chifu.
Chifu: (Kwa tabasamu) Waona sasa! Umejibu salamu visivyo. Unajua kwa nini umefikishwa hapa?
Mapunda: (Akisitasita) Si… sina ufahamu, Bwana Chifu.
Chifu: Umefikishwa hapa kwa kosa la kuiba kuku wa jirani yako, Mariasa.
Mapunda: Namwomba msamaha. Wanangu walinisumbua sana wakitaka kula kitoweo cha nyama. Uchu wa kula nyama ukanisukuma kumuiba kuku wa jirani.
Chifu: Wazee pamoja na Mariasa wameamua kukusamehe kwa sharti moja: umnunulie kuku mwenye umbo na uzani sawa na yule uliyemwiba.

Andika jibu sahihi la salamu aliyopewa Mapunda na Chifu.

Answer

Sijambo.

Jibu sahihi ni "Sijambo." Chifu alimsalimia Mapunda kwa kusema "Hujambo?", na jibu la salamu hiyo ni "Sijambo." Mapunda alijibu kwa kusema "Mimi ni mzima", jibu lisilolingana na salamu hiyo, ndiyo maana Chifu akasema, "Umejibu salamu visivyo." Kumbuka: "Hujambo?" hujibiwa "Sijambo", na "Hamjambo?" hujibiwa "Hatujambo."

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 6 Kiswahili questions from this test