naQonda

CBC Grade 8 Kiswahili School Based Assessment 2025 · Question 3

Kulingana na kifungu, wazee wa kijiji cha Mwangaza walichukua hatua gani kurejesha mshikamano?

From Kiswahili — KJSEA Assessment 2025 (Set 11) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 1 hadi 6.
Katika kijiji cha Mwangaza, wanakijiji walijulikana kwa mshikamano wao wa kipekee. Walishirikiana katika kazi za kilimo, ujenzi wa nyumba, na hata malezi ya watoto. Waliheshimu wazee na kufuata mila na desturi zao kwa uaminifu. Katika kila tukio la kijamii, kama vile harusi au mazishi, walihudhuria kwa wingi na kusaidiana kwa hali na mali.
Hata hivyo, hali hii ilianza kubadilika vijana walipoanza kuvutiwa na maisha ya mijini. Wengi walihamia mijini kutafuta ajira na kusahau desturi za jamii yao. Vijana waliobaki kijijini walikosa nidhamu na kuiga tabia zisizofaa kutoka kwa wageni waliotembelea kijiji hicho. Matumizi ya simu na mitandao ya kijamii pia yaliathiri pakubwa mawasiliano ya ana kwa ana.
Licha ya changamoto hizi, wazee wa kijiji cha Mwangaza hawakukata tamaa. Walianza kufanya mikutano ya kijamii ili kuwafundisha vijana umuhimu wa mshikamano na maadili mema. Pia, walihimiza wazazi kuwafundisha watoto wao mila na desturi tangu utotoni. Kwa juhudi hizi, taratibu kijiji kilianza kurejelea mshikamano wake wa awali.

Mchoro wa wanakijiji wengi wakishirikiana kazini mbele ya nyumba za kijiji

3. Kulingana na kifungu, wazee wa kijiji cha Mwangaza walichukua hatua gani kurejesha mshikamano?

  1. AWalihamia mijini kuwafuatilia vijana.
  2. BWaliwazuia vijana kusafiri nje ya kijiji.
  3. CWalifanya mikutano ya kijamii na kuhimiza malezi mema.
  4. DWaliwaadhibu vijana waliopoteza maadili.

Answer

C. Walifanya mikutano ya kijamii na kuhimiza malezi mema.

Aya ya tatu.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 8 Kiswahili questions from this test