CBC Grade 8 Kiswahili School Based Assessment 2025 · Question 5
Kwa mujibu wa kifungu, ni hatua gani inaweza kusaidia kudumisha mshikamano wa kijiji?
From Kiswahili — KJSEA Assessment 2025 (Set 11) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 1 hadi 6.
Katika kijiji cha Mwangaza, wanakijiji walijulikana kwa mshikamano wao wa kipekee. Walishirikiana katika kazi za kilimo, ujenzi wa nyumba, na hata malezi ya watoto. Waliheshimu wazee na kufuata mila na desturi zao kwa uaminifu. Katika kila tukio la kijamii, kama vile harusi au mazishi, walihudhuria kwa wingi na kusaidiana kwa hali na mali.
Hata hivyo, hali hii ilianza kubadilika vijana walipoanza kuvutiwa na maisha ya mijini. Wengi walihamia mijini kutafuta ajira na kusahau desturi za jamii yao. Vijana waliobaki kijijini walikosa nidhamu na kuiga tabia zisizofaa kutoka kwa wageni waliotembelea kijiji hicho. Matumizi ya simu na mitandao ya kijamii pia yaliathiri pakubwa mawasiliano ya ana kwa ana.
Licha ya changamoto hizi, wazee wa kijiji cha Mwangaza hawakukata tamaa. Walianza kufanya mikutano ya kijamii ili kuwafundisha vijana umuhimu wa mshikamano na maadili mema. Pia, walihimiza wazazi kuwafundisha watoto wao mila na desturi tangu utotoni. Kwa juhudi hizi, taratibu kijiji kilianza kurejelea mshikamano wake wa awali.

5. Kwa mujibu wa kifungu, ni hatua gani inaweza kusaidia kudumisha mshikamano wa kijiji?
- AKuwazuia vijana kusafiri kwenda mijini.
- BKuhimiza vijana kufuata mila na desturi.
- CKupunguza matumizi ya mitandao ya kijamii.
- DKuwapa vijana adhabu kali wanapokosa maadili.
Answer
B. Kuhimiza vijana kufuata mila na desturi.
Wazee walihimiza mila na desturi.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- Neno "mshikamano" limetumika katika kifungu. Kisawe cha neno hilo ni:Question 6
- Chagua jibu linaloonyesha kuwa Kunguru na Njiwa walikuwa marafiki wa dhati.Question 7
- Kwa mujibu wa kifungu, ni kwa nini Kunguru na Njiwa walihama msituni?Question 8
- Kifungu kimebainisha kuwa Kunguru ni mtu wa aina gani?Question 9
- Unaweza kusema nini kuhusu Njiwa kutokana na hadithi hii?Question 10
- Matukio yafuatayo yalitokea katika kifungu. (i) Kunguru alikamatwa. (ii) Kunguru na Njiwa walihama msituni. (iii)…Question 11