CBC Grade 8 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 15
Chagua jibu ambalo ni sahihi kwa mujibu wa kifungu.
From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 6) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali ya 13 hadi 17.
Mazingira bora ni kiini cha uhai na afya ya kila kiumbe duniani. Mahitaji ya kimsingi kama vile hewa safi, maji ya kunywa, na ardhi yenye rutuba yanategemea jinsi tunavyoyatunza mazingira yetu. Swali kuu ni, nani anayepaswa kubeba mzigo wa kuhakikisha kuwa mazingira yanahifadhiwa kwa manufaa ya wote?
Makundi mbalimbali katika jamii huchangia katika uhifadhi huu kwa njia tofauti. Watoto, kwa mfano, hufundishwa umuhimu wa kupanda miti na kutupa taka mahali panapostahili na walimu au wazazi wao. Kwa upande mwingine, viongozi wa kijamii na serikali wana jukumu la kuweka sera zinazozuia uharibifu wa misitu na vyanzo vya maji ili kulinda kizazi cha sasa na kijacho.
Kuna mambo mengi yanayoweza kukwamisha upatikanaji wa mazingira safi. Mambo hayo ni pamoja na ongezeko la viwanda na ukosefu wa elimu ya kutosha kuhusu ikolojia. Jamii inayojali mustakabali wake huweka sheria kali dhidi ya uchafuzi wa hali ya hewa. Taratibu hizi huwasaidia wanajamii kuepukana na magonjwa yanayotokana na mazingira machafu, kama vile kipindupindu na matatizo ya kupumua.
Mazingira yanapoharibiwa, jamii hukumbwa na majanga ya kimaumbile kama ukame na mafuriko. Watu huanza kupoteza makao na rasilimali zao muhimu, hali inayopelekea utegemezi na umaskini. Baadhi ya watu wenye uwezo mkubwa wa kifedha huishia kunufaika kwa kutumia vibaya maliasili zilizobaki huku wanyonge wakitaabika. Kuharibu mazingira ni sawa na kujiandalia mauti wewe mwenyewe. Ni kuifanya dunia kuwa mahali pasipofaa kuishi na kuwanyima viumbe wengine haki yao ya asili. Jamii iliyostirika ni ile inayothamini utulivu wa mazingira na kuyalinda kwa hali na mali.
15. Chagua jibu ambalo ni sahihi kwa mujibu wa kifungu.
- AJamii ikikosa kuhifadhi mazingira, utajiri huongezeka.
- BWanajamii hupata habari kuhusu mazingira kupitia mafunzo.
- CSheria za mazingira hutungwa na watoto shuleni.
- DUharibifu wa mazingira hutegemea hali ya hewa pekee.
Answer
B. Wanajamii hupata habari kuhusu mazingira kupitia mafunzo.
Watoto hufundishwa na walimu na wazazi.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- Ukiukaji wa taratibu za kuhifadhi mazingira husababishaQuestion 16
- Kulingana na kifungu, maana ya neno ‘mustakabali’ niQuestion 17
- Chagua jibu linaloonyesha klabu ambazo wanafunzi hukutana mara mbili pekee kwa juma.Question 18
- Ni siku gani ambayo wanafunzi wa shule ya Bidii hushiriki katika idadi ndogo zaidi ya klabu?Question 19
- Chagua jibu linaloonyesha klabu ambazo wanafunzi hushiriki siku ya Jumatano pekee.Question 20
- Chagua jibu lenye kauli sahihi kujaza nafasi ya 21 katika kifungu.Question 21