CBC Grade 8 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 8
Chagua isiyo maliasili kati ya zifuatazo.
From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 3) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 8 hadi la 13.
Je, maliasili ni nini? Maliasili ni vitu vinavyotokana na maumbile na vyenye manufaa katika maisha yetu. Mifano ya maliasili ni hewa, madini, misitu, maji na kadhalika. Ni bayana na wazi kuwa maliasili yana umuhimu mkubwa katika maisha yetu.
Misitu huchangia katika kuvutia mvua, kusafisha hewa, kutupa chakula na dawa. Aidha, misitu ni makao ya wanyamapori na viumbe wengine mbalimbali. Ni nani asiyefahamu umuhimu wa wanyamapori? Wao huvutia watalii ambao hutuletea pesa za kigeni. Misitu inafaa kulindwa ili kuwatunza wanyama na mazingira. Tujiepushe na ukataji ovyo wa miti na uharibifu wa misitu. Kukosekana kwa wanyamapori kunaweza kuiletea nchi yetu hasara kubwa.
Umuhimu wa ardhi kwetu hauwezi ukapuuzwa hata kidogo. Ardhi ndio msingi wa baadhi ya maliasili na shughuli za binadamu. Makao au makazi ya wanyama na binadamu yamejengwa ardhini. Ardhi yenye rutuba huwezesha mimea kukua na kunawiri. Hivyo, huendeleza shughuli za zaraa na upataji wa mazao tele. Vilevile, madini kama vile dhahabu, fedha na petroli hupatikana katika ardhi. Madini haya nayo hutufaa kwa njia anuwai. Ni vyema kuilinda ardhi yetu kwa kuizuia mmomonyoko wa udongo.
8. Chagua isiyo maliasili kati ya zifuatazo.
- AMadini
- BMisitu
- CMaji
- DMifereji
Answer
D. Mifereji
Mifereji hujengwa na binadamu; madini, misitu na maji hutokana na maumbile.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- Misitu huchangia katika mambo yafuatayo ilaQuestion 9
- Kunawiri kama ilivyopigiwa mstari ina maana yaQuestion 10
- Chagua jibu linaloonyesha utunzaji wa maliasili.Question 11
- Mmomonyoko wa udongo una hasara gani?Question 12
- Mada mwafaka ya kifungu hiki ni gani?Question 13
- Zuhura alikuwa na ujuzi wa kazi gani?Question 14