CBC Grade 7 Kiswahili School Based Assessment 2025 · Question 16
Ni uamuzi gani uliofanywa kuhusu hazina aliyopata Juma?
From Kiswahili — KJSEA Assessment 2025 (Set 9) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Hadithi
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali ya 13 hadi 17.
Miaka ya kale, jamii ya Waswahili iliheshimu sana bahari. Bahari ilikuwa chanzo cha riziki na njia ya kuwasiliana na mataifa ya mbali. Wavuvi walitegemea bahari kwa samaki ilhali wafanyabiashara walitumia meli kusafiri hadi nchi za kigeni kuleta bidhaa kama vile vitambaa, viungo na vyombo vya shaba.
Katika kijiji cha Pwani, aliishi kijana shupavu aitwaye Juma. Juma alikuwa mvuvi hodari aliyependa kuvua samaki kila asubuhi. Alijua mbinu zote za uvuvi na alikuwa na mashua iliyomsaidia kupenya mbali ndani ya bahari. Juma alifundishwa na babu yake, mvuvi maarufu aliyestaafu.
Siku moja, akiwa baharini, Juma aliona kitu cha ajabu kikin’garika ndani ya maji. Alipochunguza kwa karibu, aligundua kuwa ni chombo cha kale kilichojaa lulu na vito vya thamani. Juma alifurahi mno, lakini akakumbuka maneno ya babu yake: “Utajiri wa haraka huja na majaribu.”
Juma aliamua kurudi kijijini na kushauriana na wazee. Wazee walikubaliana kwamba hazina hiyo ni sehemu ya urithi wa jamii, na hivyo ilifaa itumiwe kwa manufaa ya watu wote. Kwa mshikamano, walijenga shule na soko jipya, jambo lililobadili maisha ya wanakijiji wote.
16. Ni uamuzi gani uliofanywa kuhusu hazina aliyopata Juma?
- AAliiweka kwa matumizi yake binafsi.
- BAligawana na marafiki wake wa karibu.
- CIlitumiwa kwa manufaa ya jamii.
- DIliuzwa kwa bei ya juu sokoni.
Answer
C. Ilitumiwa kwa manufaa ya jamii.
Wazee waliamua hazina itumiwe kwa manufaa ya watu wote, wakajenga shule na soko jipya.
More Grade 7 Kiswahili questions from this test
- Maana ya msemo “Utajiri wa haraka huja na majaribu” kama ilivyotumika kifunguni ni:Question 17
- Ni mteja yupi hununua aina tano tofauti za vyombo?Question 18
- Ni chombo gani hununuliwa sana na wateja wa Bi. Neema?Question 19
- Ni siku gani kila mteja hununua chombo tofauti na cha wengine?Question 20
- Amina na Baraka hununua chombo kipi kwa siku moja?Question 21
- Ni mteja yupi hununua sufuria mara nyingi zaidi?Question 22