naQonda

CBC Grade 7 Kiswahili Exam Term 1 2025 · Question 8

Taja hasara ambayo imeletwa na kompyuta. (al.1)

From Kiswahili — Extra-Activity Assessment 2025 (Set 8) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 6 hadi la 8.
Kuwepo kwa tarakilishi kumechangia pakubwa katika kukua kwa Uchumi kibiashara kuboresha, bila kusahau kurahisisha mawasiliano. Kazi zilizofanywa na watu wengi huweza kufanywa kwa kidole kimoja tu.
Zilizochukua siku nyingi zimebaki kufanyika kwa sekunde tu. Hizi ni juhudi za wanasayansi na wahandisi. Miaka imefupishwa na kuwa sekunde, nayo dunia nzima kuwa kitongoji tu. Makabila yakakusanywa Pamoja kuwa kama mlango mmoja wa ukoo.
Kumbuka uundaji wa tarakilishi ni njia ya mwanadamu kumuiga Mungu. Tarakilishi hufanya kazi nyingi. Zikiwemo kutuma ujumbe, kuhifadhi kumbukumbu, kuendesha mipango mbalimbali na kazi nyingine. Kompyuta pia ni kifaa cha burudani. Kina michezo mbalimbali ya kumstarehesha binadamu. Huweza pia kutumika kuonyesha filamu na kuonyesha muziki.
Tarakilishi imezaa madhara makubwa katika jamii. Hivi leo mfanyikazi mmoja, kwa kutumia kompyuta, anafanya kazi za watu wengi, jambo ambalo limesababisha kuachishwa kazi kwa watu wengi.

8. Taja hasara ambayo imeletwa na kompyuta. (al.1)

Answer

Watu wengi wameachishwa kazi kwa sababu mfanyikazi mmoja anafanya kazi za watu wengi.

Aya ya mwisho.

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 7 Kiswahili questions from this test