CBC Grade 7 Kiswahili Opener Exam Term 2 2026 · Question 7
Wazazi walivutiwa sana na jambo lipi?
From Kiswahili — Term 2 Opener Assessment 2026 (Set 12) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Hadithi
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 1 mpaka la 9.
Hapo jadi, paliondokea mzee aliyeitwa Tumaini. Mzee huyo alijaliwa wana wawili wa kiume. Mmoja aliitwa Fanaka na mwenzake Maisha. Mzee alijifunga mkaja ili kuwakidhia wanawe mahitaji yao yote kutokana na biashara ndogondogo alizoshiriki kila siku. Watoto nao walielewa kuwa mtaka cha mvunguni sharti ainame. Wakiwa shuleni, walifanya bidii mithili ya mchwa mwishowe wakafaulu vizuri sana.
Muda si muda, vijana wale walipata ajira katika kiwanda kimoja. Maisha alipendwa sana na waajiri wake kutokana na weledi wake kazini. Alivikwa mbeleko akawa karani wa mauzo hapo kazini.
Wahenga walisema hakuna kizuri kisichokuwa na ila. Licha ya ujuzi wake wa kazi, Maisha alikuwa mbadhirifu. Mshahara wake haukufanikiwa kuona tarehe tano ya mwezi. Alizoea kufuja pesa zake kwa starehe za kila nui. Ndugu yake, Fanaka, aliwahi kujaribu kumshika sikio dhidi ya hulka hiyo lakini wapi! Je, sikio la kufa limewahi kusikia dawa kweli?
Kwa upande wa Fanaka, licha ya kupata mshahara wa wastani, aliutumia kwa uwajibikaji. Kila mwezi, mbali na kukidhi mahitaji yake, aliwatumia wazazi wake kiasi fulani cha pesa na kuweka fulusi nyingine kama akiba benkini. Hata alijijengea nyumba ya aushi pale kijijini ili apate mahali pa kurejea iwapo mambo yangemwendea mrama.
Wakati mmoja biashara iliharibika sana hivi kwamba kiwanda walichofanyia kazi vijana wale hakikuwa na budi kufungwa. Machozi ya majonzi yalimbubujika Maisha bububu. Hakujua aanzie wapi wala amalizie wapi. Wafanyakazi wote wakamwaga unga pale kiwandani.
Ng’ombe akivunjika mguu malishoni hujikokota zizini kusaidiwa. Fanaka na Maisha walifunganya virago vyao wakarejea kijijini. Wazazi wao, ambao sasa uzee ulikuwa umeanza kuwalemea, hawakuwa na njia ya kuwafaa.
Fanaka hakuwa na wasiwasi. Yeye alishajua kitambo kuwa akiba haiozi. Aliitumia akiba yake kama mtaji akaanzisha miradi ya kilimo na ufugaji hapo nyumbani. Isitoshe, kwa kuelewa kuwa damu ni nzito kuliko maji, alimtafutia kakaye karadhi ili aanzishe shughuli za kujitegemea. Wazazi walifurahi sana walipoona kuwa watoto wanajaliana maslahi. Maisha naye akaona umuhimu wa kujiwekea akiba.
Jamaa ile ilimiminiwa neema na Maulana. Mali kwao ikawa inaoza na kuozeana. Vijana wengine walifuata mfano huo, wakaanzisha miradi ya kujitegemea badala ya kung’ang’ania kazi za ajira ambazo zilikuwa wali wa daku.
7. Wazazi walivutiwa sana na jambo lipi?
- Akuwaona watoto wakisaidiana
- Bwatoto kurudi nyumbani
- Cbiashara walizoanzisha watoto
- Dmaisha kumsaidia ndugu yake
Answer
A. kuwaona watoto wakisaidiana
"Wazazi walifurahi sana walipoona kuwa watoto wanajaliana maslahi."
More Grade 7 Kiswahili questions from this test
- Kichwa kifaacho zaidi kwa hadithi hii niQuestion 8
- Neno 'kufuja' limetumiwa katika kifungu hiki. Neno hilo lina maana sawa naQuestion 9
- Kulingana na aya ya kwanzaQuestion 10
- Matokeo ya kutofuata maadili katika jamii huwaQuestion 11
- Ni sahihi kusema kuwaQuestion 12
- Kwa jumla, kifungu hiki kinatoa wito kwa wazazi kuwaQuestion 13