CBC Grade 7 Kiswahili School Based Assessment 2025 · Question 8
ZOEZI III: NOVELA (Alama 10) (a) Kazi za fasihi huwa na malengo maalum. Eleza dhamira ya sehemu hii ya novela. (alama 2)
From Kiswahili — KJSEA Series July–August 2025 (Set 12) · 2 marks · Topic: Kusoma, Novela
3. Soma sehemu ifuatayo ya novela kisha ujibu maswali.
Jua lilichomoza taratibu, likiangazia kijiji cha Umoja. Kila alfajiri, sauti ya jogoo ilikuwa ishara ya kuanza kwa shughuli mpya. Bwana Tenge, baba wa Tumaini, aliamka mapema kama kawaida. Alikuwa akifanya kazi shambani bila kuchoka, akipambana na udongo mgumu na jua kali ili kuhakikisha familia yake inakula. Tumaini, binti yake pekee, alikuwa nuru ya macho yake. Aliamini kuwa elimu ndiyo ufunguo wa maisha bora.
Tumaini alikuwa mwanafunzi mwenye bidii sana. Tangu akiwa mdogo, alipenda kusoma vitabu na hakuwahi kukosa nafasi ya kujifunza jambo jipya. Alikuwa akisaidia mama yake, Bi. Zawadi, katika kazi za nyumbani baada ya kurudi shuleni. Mama Zawadi alimhimiza sana katika masomo, akimwambia, "Elimu ni urithi bora kuliko mali, binti yangu." Maneno haya yalimtia moyo Tumaini kujitahidi zaidi.
Hata hivyo, familia ya Bwana Tenge ilikabiliwa na changamoto nyingi. Bei za mazao zilishuka ghafla, na wakulima wengi walilalamika. Bwana Tenge alijitahidi kudumisha matumaini, lakini mara nyingi alihisi kuzidiwa na mzigo wa maisha. Alianza kufikiria kuacha shamba na kuhamia mjini kutafuta kazi. Mawazo haya yalimsumbua sana, hasa alipomwangalia Tumaini ambaye alikuwa akisubiri matokeo yake ya mitihani ya kitaifa.
Siku ya matokeo ilifika. Familia nzima ilikuwa na wasiwasi. Tumaini alikuwa ametumia usiku kucha akisali. Alipata matokeo, machozi ya furaha yalimtiririka. Alikuwa amefaulu vizuri sana, na alikuwa mwanafunzi bora katika wilaya nzima. Habari zilienea kama moto wa nyasi. Watu kutoka vijiji jirani walikuja kupongeza familia ya Bwana Tenge. Viongozi wa serikali na mashirika mbalimbali waliahidi kumsaidia Tumaini kuendelea na masomo yake. Familia ilipata msaada wa kujenga nyumba mpya na kupata rasilimali za kutosha za kilimo. Matokeo ya Tumaini yalionyesha kuwa elimu inaweza kuleta mabadiliko makubwa katika maisha ya jamii.
ZOEZI III: NOVELA (Alama 10)
(a) Kazi za fasihi huwa na malengo maalum. Eleza dhamira ya sehemu hii ya novela. (alama 2)
Answer
Dhamira ni kuonyesha kuwa elimu ni ufunguo wa maisha bora na inaweza kubadilisha maisha ya familia na jamii, na kuwa bidii hushinda changamoto.
Mafanikio ya Tumaini katika mtihani yaliibadilisha familia yake: mwandishi anaonyesha umuhimu wa elimu na bidii.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 7 Kiswahili questions from this test
- (b) Eleza aina mbili za mandhari zinazojitokeza katika sehemu hii ya novela. (alama 2)Question 9
- (c) Tumaini ni mwenye bidii masomoni. Eleza sifa nyingine mbili za Tumaini. (alama 2)Question 10
- (d) Ploti ni namna ambavyo matukio katika kazi ya fasihi yanavyojitokeza. Eleza mfuatano wa matukio katika maisha ya…Question 11
- (e) Eleza mbinu mbili za lugha zilizotumiwa katika sehemu hii ya novela. (alama 2)Question 12
- ZOEZI LA IV: TAMTHILIA (Alama 10) (a) Mazungumzo ni mojawapo ya sifa za tamthilia. Eleza sifa nyingine mbili za…Question 13
- (b) Mada ya usafi wa mazingira imeshughulikiwa katika sehemu hii ya tamthilia. Fafanua mada nyingine mbili ambazo…Question 14