naQonda

CBC Grade 7 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 2

Mawazo ya Musa, "Kuna mtoto mtoni?" yanadhihirisha nini kuhusu jamii yake?

From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 5) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali ya 1 hadi 6.
Musa alitembea kwa haraka akitoka shuleni kuelekea nyumbani. Siku hiyo alikuwa amechoka sana baada ya kushiriki katika mashindano ya riadha. Alitamani kufika mapema ili apate muda wa kupumzisha mwili wake. Alipokuwa akipita kando ya mto mdogo, ghafla alisikia sauti ya mtoto ikilia kwa unyonge. "Huwezi amini! Kuna mtoto mtoni?" Musa alijiuliza kwa mshtuko mkubwa huku moyo wake ukidunda kwa kasi. Alisogea polepole na kuchungulia kando ya maji. Alipigwa na bumbuazi kumwona mtoto mchanga ameachwa ndani ya sanduku kuukuu kando ya mwanzi.
Musa alitaka kutoroka kwa hofu, lakini alipoangalia vizuri, aliona mamba mdogo akikaribia sanduku lile. Mamba huyo alikuwa ametulia tuli kama maji ya mtungi akisubiri mawindo. Bila woga, Musa alinyakua sanduku lile na kukimbia nalo upesi. Alifika nyumbani akitweta na kuwaeleza wazazi wake kila kitu. Mama yake alimshughulikia yule mtoto kwa upendo, huku baba na Musa wakielekea kituo cha polisi kutoa ripoti.

2. Mawazo ya Musa, "Kuna mtoto mtoni?" yanadhihirisha nini kuhusu jamii yake?

  1. AWatoto wengi hupenda kuchezea mtoni.
  2. BNi hatari sana kutembea kando ya mito.
  3. CSio kawaida kumpata mtoto ameachwa mtoni.
  4. DWanafunzi wengi hawapendi kukaa shuleni.

Answer

C. Sio kawaida kumpata mtoto ameachwa mtoni.

Alishtuka kwa sababu si jambo la kawaida.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 7 Kiswahili questions from this test