CBC Grade 7 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 3
Neno asteaste kama ilivyotumika katika ufahamu huu ni kisawe cha
From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 4) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma ufahamu ufuatao kisha ujibu swali 1-7
Utamanduni ni mila, asili, jadi na desturi za kundi la jamii fulani. Katika karne moja hivi iliyopita makabila mbalimbali yamekuwa yakiacha kuzifuata tamaduni zao aste aste. Hususan katika miongo mitano ya mwisho wa karne hiyo kulishudiwa mabadiliko makubwa ya kijamii. Huenda haya yalisababishwa na kuingia kwa mkoloni aliyedumisha utamaduni wa mwafrika akiuita upumbavu.
Hata hivyo kunayo makabila ambayo yalikataa katakata kuziachilia tamaduni zao na bado mpaka leo wanazishlalia kikiki. Sitaki kusema kuwa tamaduni zetu zlikuwa mbaya. Asilimia kubwa ya tamanduni hizi zilifaa sana. Mifano ni jinsi chipukizi walivyofunzwa maadili na kina nyanya, shangazi, halati na kadhalika. Zama za leo hakuma mpango wowote uliowekwa wa kuwafunza vijana. Wameachiwa kujifunza kutoka kwenye runinga, magazeti, mitandao na hata majarida.
Matokeo ya kutofunzwa nayo yamekuwa yakufedhesha na ya kuvunja moyo. Mavazi, mitindo ya kusakata rumba, lugha na kadhalika yale yamekuwa uvundo mtupu. Angalia hata michezo ya kuigiza katika vyombo vya mawasiliano. Mambo ambayo yalikuwa mwiko yameanikwa na vijana wetu mbele ya wavyele na wana wao sebuleni. Utawaona vijana wetu wameshikana mabega na hata kupigana busu hadharani eti ni maendeleo. Kumbe hayo yote yameigwa kutoka nchi zilizoendelea.
Sisemi turudie utamaduni. Lo, ninachojaribu kusema ni kuwa yatupasa kuudumisha utamaduni wa mwafrika. Tujivunie utamaduni wetu kwa nini tukubali kuiga tamaduni za wazungu? Tunapovutiwa na tamaduni zao yaonyesha dhahiri shairi kuwa tungali tunatawaliwa na wenzangu waliotuonyesha kuwa mwafrika hana chake.
3. Neno asteaste kama ilivyotumika katika ufahamu huu ni kisawe cha
- Aharakaharaka
- Bpolepole
- Cupesiupesi
- Dutaratibu
Answer
B. polepole
Asteaste ni polepole.
More Grade 7 Kiswahili questions from this test
- Ni nini kilisababisha mabadiliko ya utamaduni wa mwafrika?Question 4
- Wote hawa wemetajwa kama waliohusika katika kuwafunza chipukizi maadili isipokuwaQuestion 5
- Ni nini kimewafanya vijana kuiga desturi za wazungu?Question 6
- Mwandishi anaomba tufanye nini katika aya ya mwisho?Question 7
- Kifungu kimebainisha kuwa kobeQuestion 8
- Kunguru alimpa kobe nini?Question 9