naQonda

CBC Grade 7 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 6

Ni jukumu la nani kuhifadhi mazingira?

From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 1) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 1 hadi la 6.
Wanyama pori ni sehemu muhimu ya mfumo wa ikolojia na utalii. Baadhi yao ni wakubwa na wenye nguvu kama simba, chui na tembo. Wengine ni wadogo na wa haraka kama swala na sungura. Kila mnyama ana jukumu lake katika mazingira. Simba husaidia kudhibiti idadi ya wanyama wengine, na hivyo kuzuia mazingira kuharibika. Nyuki na vipepeo, ingawa ni wadogo, huchangia pakubwa katika uchavushaji wa mimea.
Wanyama hawa wanakabiliwa na changamoto nyingi. Ujangili, au uwindaji haramu, ni tishio kubwa. Wengine wanatafutwa kwa pembe zao au meno yao, na hivyo kupelekea idadi yao kupungua. Uharibifu wa misitu na makazi yao pia unawaathiri vibaya. Serikali na mashirika mbalimbali yameanzisha hifadhi za wanyama na mbuga za kitaifa ili kuwalinda. Elimu kuhusu umuhimu wa wanyama pori inahitajika ili kila mtu aelewe jukumu lake katika uhifadhi.

6. Ni jukumu la nani kuhifadhi mazingira?

  1. AMashirika
  2. BSerikali
  3. CKila mmoja
  4. DWanyama

Answer

C. Kila mmoja

Kifungu kinasema kila mtu aelewe jukumu lake katika uhifadhi.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 7 Kiswahili questions from this test