naQonda

CBC Grade 7 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 6

Ni nini kilichomfanya Sungura kushindwa shindano? (Alama 2)

From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 1) · 2 marks · Topic: Kusoma, Fasihi Simulizi

SEHEMU B (ALAMA 35)
ZOEZI LA II: FASIHI SIMULIZI (alama 10)
Soma sehemu ifuatayo ya fasihi simulizi kisha ujibu maswali.
Hapo zamani za kale, Kobe na Sungura walikuwa majirani. Sungura alikuwa na kiburi sana na alijisifu kwamba yeye ndiye mnyama mwenye kasi zaidi msituni. Kobe alikuwa mnyama mpole na hakupenda kujisifu.
Siku moja, Sungura alimcheka Kobe kwa mwendo wake wa polepole. “Hahahaha! Kobe, wewe unatembea kama umefungiwa minyororo! Mimi ninaweza kukimbia kuzunguka msitu mara kumi kabla wewe hujasogea hatua moja!” Sungura alicheka. Kobe alihuzunika, lakini akasema kwa utulivu, “Sungura, mwendo sio kila kitu. Tushindane kuona ni nani atafika upande ule mwingine wa msitu kwanza.” Sungura alicheka zaidi.
“Wewe Kobe? Kushindana nami? Haya, niko tayari!” Walikubaliana kuanza shindano asubuhi iliyofuata. Walipokutana, wanyama wengine wengi walikusanyika kuwashuhudia. Sungura alikuwa amejiamini sana. Shindano lilipoanza, Sungura alitimua mbio kwa kasi ya ajabu. Alijua Kobe alikuwa polepole sana. Alipokuwa katikati ya njia, Sungura alifikiri, “Kobe bado yuko mbali sana. Nitapumzika kidogo chini ya mti huu.”
Alijilaza na usingizi mzito ukamchukua. Wakati huohuo, Kobe aliendelea kutembea polepole, hatua kwa hatua, bila kusimama. Alipofika karibu na alikokuwa Sungura, alimwona amelala fofofo. Kobe hakumwamsha. Aliendelea na safari yake polepole lakini kwa uhakika. Alipofika mwisho wa njia, wanyama wengine walimshangilia kwa nguvu. Kelele hizo zilimwamsha Sungura, akafumbua macho na kukimbia kwa kasi, lakini ilikuwa imechelewa. Kobe alikuwa tayari ameshafika. Sungura aliona aibu na akafunika uso wake.
Tangu siku hiyo, Sungura alijifunza kuwa kiburi si kizuri na mwendo wa polepole pia huweza.

5. Ni nini kilichomfanya Sungura kushindwa shindano? (Alama 2)

Answer

Alijiamini kupita kiasi akalala chini ya mti katikati ya njia, akapitwa na Kobe.

Sungura alifanya nini katikati ya njia?

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 7 Kiswahili questions from this test