CBC Grade 7 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 11
Mazungumzo haya yalifanyiwa wapi? (Alama 2)
From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 1) · 2 marks · Topic: Kusoma, Tamthilia
ZOEZI LA IV: TAMTHILIA (Alama 10)
Soma sehemu ifuatayo ya tamthilia kisha ujibu maswali.
SEHEMU 1 Onyesho 1
(Ndani ya duka dogo la kijijini. Bibi mwanza anakaa nyuma ya rafu , akifuta fumbo. Mjukuu wake, Ali, mwanafunzi wa gredi ya 7, anaingia akitokea shuleni, begani amebeba mkoba wa vitabu.)
ALI : Shikamoo bibi!
BIBI MWANZA : (Akiinua kichwa na kutabasamu) Marahaba mjukuu wangu. Karibu nyumbani. Habari za shule?
ALI : Nzuri sana bibi. Leo mwalimu alitufundisha hesabu. Nilielewa vizuri!
BIBI MWANZA : Heko! Hiyo ndiyo kazi, mwanangu. Bidii katika masomo.?Nikuandalie kitu?
ALI : Njaa kidogo bibi. Ningependa chai kwa maandazi kama yapo.
BIBI MWANZA : Maandazi yameisha. Lakini nina viazi vitamu vimechemshwa. Vile unapenda. Nikuandalie?
ALI : (Akifurahi) Ndiyo bibi! Ninavipenda sana! Asante bibi!
BIBI MWANZA : Haya, nenda kwanza ukaweke begi lako na unawe mikono. Mimi nakuandalia hapa.
ALI : Sawa bibi. (Ali anaondoka kuelekea sebuleni.)
(Bibi Mwanza anatabasamu akitazama njia alikoenda Ali. Anachukua sahani na kuanza kuandaa viazi vitamu. Mlango wa duka unafunguliwa tena, na jirani, Mama Sara, anaingia.)
MAMA SARA : Habari za jioni Bibi Mwanza! Nimekuja kuchukua mafuta ya taa.
BIBI MWANZA : Karibu Mama Sara! Njema tu. Mafuta yapo. Unataka kiasi gani?
MAMA SARA : Chupa moja tu, ahsante. Nimeona Ali amerudi shuleni. Amekuwa mkubwa sana!
BIBI MWANZA : (Akijivunia) Ndiyo, Mungu anamkuza. Anajitahidi sana shuleni. Tumaini langu yeye.
MAMA SARA : Mungu ambariki. Elimu ndiyo kila kitu siku hizi. Najua hata msikitini yuko sawa.
10. Mazungumzo haya yalifanyiwa wapi? (Alama 2)
Answer
Ndani ya duka dogo la kijijini (la Bibi Mwanza).
Soma maelezo ya jukwaa mwanzoni.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 7 Kiswahili questions from this test
- Taja wahusika watatu wakuu katika sehemu hii ya tamthilia. (Alama 3)Question 12
- Lengo la Mama Sara lilikuwa gani? (Alama 2)Question 13
- Mbali na dukani, andika mahali kwingine tatu kulikotajwa katika mazungumzo haya. (Alama 3)Question 14
- Andika ujumbe wa ubeti wa mwisho (Alama 2)Question 15
- Shairi hili lina beti ngapi? (Alama 2)Question 16
- Shairi hili ni la Bahari gani? (Alama 1)Question 17